Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 98

98
Zaburi 98
Mwenyezi Mungu Mtawala wa dunia
Zaburi.
1Mwimbieni Mwenyezi Mungu wimbo mpya,
kwa maana ametenda mambo ya ajabu;
kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu
umemfanyia wokovu.
2Mwenyezi Mungu ameufanya wokovu wake ujulikane
na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.
3Ameukumbuka upendo wake
na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;
miisho yote ya dunia imeuona
wokovu wa Mungu wetu.
4Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote,
ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
5mwimbieni Mwenyezi Mungu kwa kinubi,
kwa kinubi na sauti za kuimba,
6kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume:
shangilieni kwa furaha mbele za Mwenyezi Mungu, aliye Mfalme.
7Bahari na ivume na kila kilicho ndani yake,
dunia na wote wanaoishi ndani yake.
8Mito na ipige makofi,
milima na iimbe pamoja kwa furaha,
9vyote na viimbe mbele za Mwenyezi Mungu,
kwa maana yuaja kuhukumu dunia.
Atahukumu dunia kwa haki
na mataifa kwa haki.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 98: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia