Ufunuo 22:6-11
Ufunuo 22:6-11 NENO
Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Mwenyezi Mungu, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.” “Tazama, naja upesi! Amebarikiwa yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.” Mimi, Yohana, ndiye niliyesikia na kuyaona mambo haya. Nilipokwisha kuyasikia na kuyaona, nilianguka chini nikasujudu miguuni pa yule malaika aliyekuwa akinionesha mambo hayo. Lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi ni mtumishi pamoja nawe na ndugu zako manabii na wote wanaoyashika maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu!” Kisha akaniambia, “Usiyafunge maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, kwa sababu wakati umekaribia. Atendaye mabaya na aendelee kutenda mabaya, aliye mchafu na aendelee kuwa mchafu, yeye atendaye haki na aendelee kutenda haki, na yeye aliye mtakatifu na aendelee kuwa mtakatifu.”