Warumi 16:21-27
Warumi 16:21-27 NENO
Timotheo, mtendakazi mwenzangu anawasalimu. Vivyo hivyo Lukio, Yasoni, na Sosipatro, ndugu zangu. Mimi, Tertio, niliye mwandishi wa waraka huu, nawasalimu katika Bwana Isa. Gayo, ambaye ni mwenyeji wangu na wa kundi lote la waumini, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto ndugu yetu, pia wanawasalimu. [ Neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe pamoja nanyi nyote. Amen.] Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Isa Al-Masihi, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale. Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii: ndiye Mungu, aliye pekee mwenye hekima, ambaye kupitia kwa Isa Al-Masihi utukufu ni wake milele na milele! Amen.