1 Kor 10
10
Maonyo kutoka kwa Historia ya Israeli
1 #
Kut 13:21-22; 14:22-29 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3#Kut 16:4,35; Kum 8:3wote wakala chakula kile kile cha roho; 4#Kut 17:6; Hes 20:11wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5#Hes 14:16,23,29-30Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. 6#Hes 11:4,34Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. 7#Kut 32:6Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8#Hes 25:1-18Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. 9#Hes 21:5-6Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. 10#Hes 16:41-49; 14:2,36; Ebr 3:11,17Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. 11#1 Pet 4:7Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. 13Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
14 #
1 Yoh 5:21
Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. 16#Mt 26:26-28; Mk 14:22-24; Lk 22:19-20; Mdo 2:42Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17#1 Kor 12:27; Rum 12:5Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18#Law 7:6,15Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19#1 Kor 8:4Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20#Kum 32:17; Law 17:7; Zab 106:37; Ufu 9:20Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21#2 Kor 6:15,16; Mal 1:7,12Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22#Kum 32:21Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?
Fanyeni yote kwa Utukufu wa Mungu
23 #
1 Kor 6:12
Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo. 24#Rum 15:2Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake. 25#1 Kor 14:2-10,22Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; 26#Zab 24:1maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo. 27#Lk 10:8Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri. 28#1 Kor 8:7Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri. 29Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 30#1 Tim 4:4Ikiwa mimi natumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho? 31#Kol 3:17Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. 32#Rum 14:13Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu, 33#1 Kor 9:20-22vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa. a.
Iliyochaguliwa sasa
1 Kor 10: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.