Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Fal 5

5
Maandalizi ya vifaa vya Kujengea Hekalu
1 # 2 Sam 5:11; Amo 1:9 Ndipo Hiramu, mfalme wa Tiro, akawatuma watumishi wake kwa Sulemani; kwani alikuwa amesikia ya kwamba wamemtia mafuta awe mfalme mahali pa baba yake. Kwa maana Hiramu alikuwa akimpenda Daudi siku zote. 2#2 Nya 2:3Basi Sulemani akatuma watu kwa Hiramu, akasema, 3#2 Sam 7:5; 1 Nya 22:8; 28:3; 2 Nya 6:6-8Umemjua Daudi baba yangu jinsi asivyoweza kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata BWANA alipowatia watu chini ya nyayo zake. 4#1 Nya 22:9; Zab 72:7; Isa 9:7Ila leo BWANA, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui, wala tukio baya. 5#2 Nya 2:4; 2 Sam 7:12,13; 1 Nya 22:10Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wangu, kama BWANA alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. 6#1 Fal 6:9,10,16,20; 2 Nya 2:8; Eze 27:5Basi uamuru wanikatie mierezi ya Lebanoni; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni. 7Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe BWANA leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi. 8Hiramu akatuma watu kwa Sulemani, akasema, Nimeyasikia yale uliyoniletea; nami nitafanya kila ulitakalo katika habari ya miti ya mierezi, na miti ya miberoshi. 9#1 Fal 9:20,21; 2 Nya 2:16; Ezr 3:7; Eze 27:17; Mdo 12:20Watumishi wangu wataishusha toka Lebanoni mpaka baharini; nami nitaiendesha baharini, ikifungwa pamoja, mpaka mahali utakaponiagiza, huko nitaifungua ili wewe uichukue; ndivyo utakavyoitimiza haja yangu, ukiwapa chakula watu wa nyumbani mwangu. 10Basi Hiramu akampa Sulemani miti ya mierezi na miti ya miberoshi kadiri alivyotaka. 11#2 Nya 2:10Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano, chakula cha watu wake, na kori ishirini za mafuta safi. Ndizo Sulemani alizompa Hiramu mwaka kwa mwaka. 12#1 Fal 3:12; 2 Nya 1:12; Yak 1:5BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanyana maagano pamoja hao wawili.
13Mfalme Sulemani akafanya shokoa ya Israeli wote; nayo shokoa hiyo ilikuwa ya watu thelathini elfu. 14#1 Fal 12:18Akawatuma Lebanoni kwa mwezi, elfu kumi kwa zamu. Mwezi mmoja walikuwako huko Lebanoni, na miezi miwili wakawako kwao. Na Adoramu alikuwa juu ya shokoa. 15Sulemani alikuwa na wachukua mizigo sabini elfu, na wakatao miti themanini elfu milimani; 16mbali na maakida yake Sulemani waliokuwa juu ya kazi, elfu tatu na mia tatu, wasimamizi wa watu waliotenda kazi. 17Mfalme akaamuru, nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa. 18Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.

Iliyochaguliwa sasa

1 Fal 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia