Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Sam UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kuna vitabu viwili vya Samweli. Vitabu hivi vilikuwa kitabu kimoja katika Biblia ya zamani ya Kiebrania. Baadaye kiligawanywa na kuwa vitabu viwili - cha Kwanza na cha Pili. Ijapokuwa vitabu hivi vinaitwa vya Samweli kuna habari chache zinazomhusu Samweli. Vile vile Samweli hakuandika habari nyingi zilizomo vitabuni humu ila sehemu chache tu, sehemu nyingine zimeandikwa na watu wengine (1 Sam 10:25; 2 Sam 1:18; 1 Nya 27:24; 29:29). Samweli alikuwa nabii na mwamuzi wa mwisho katika Israeli. Alipaka mafuta wafalme Sauli na Daudi.
Kitabu cha Kwanza cha Samweli kinasimulia historia ya Samweli na jinsi Waisraeli walivyowashinda Wafilisti, Sanduku la BWANA likatekwa. Hata hivyo Mungu aliwarudishia Waisraeli Sanduku lake. Waisraeli walitaka wawe na mfalme, Sauli akateuliwa akawa mfalme wao wa kwanza. Sauli hakuwa mwaminifu kwa Mungu. Ndipo akateuliwa mfalme wao wa pili aitwaye Daudi. Mkazo wa masimulizi haya ni umoja wa kidini na kitaifa wenye kumtii Mungu.
Yaliyomo:
1. Habari juu ya mwamuzi wa mwisho, Samweli, Sura 1–7
2. Kuanzishwa uongozi wa kifalme, Sura 8–10
3. Utawala wa Sauli, Sura 11–15
4. Simulizi juu ya Sauli na Daudi, Sura 16–30
5. Kifo cha Sauli na wanawe, Sura 31

Iliyochaguliwa sasa

1 Sam UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia