2 Yoh UTANGULIZI
UTANGULIZI
Yohana alipata habari kuwa waalimu wa uongo waliendeleza mafundisho yao katika Kanisa; hivyo akaandika Waraka huu kuagiza Wakristo wajitenge na walimu wa uongo na wasiwakaribishe katika ibada zao.
Mwandishi anajiita “Mzee” anayemwandikia “Bimkubwa” mteule pamoja na “Wanawe”. Mwandishi wa Waraka huu ni Yohana ambaye wakati huo, kiumri, alikuwa mzee aliyeheshimiwa kama kiongozi wa Kanisa (tazama utangulizi wa Waraka wa Kwanza wa Yohana). Walengwa wa Waraka huu ni Kanisa fulani katika Asia Ndogo lililokuwa chini ya uongozi wake. Limepewa jina la heshima la “Bimkubwa mteule.” “Watoto wake” ni waumini waliokuwa katika Kanisa hilo.
Mwandishi anawatahadharisha waumini waepuke mafundisho ya uongo, wazingatie imani, ukweli na upendo.
Iliyochaguliwa sasa
2 Yoh UTANGULIZI: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.