Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Fal 11

11
Malkia Athalia Atawala Yuda
1 # 2 Nya 22:10; 2 Fal 8:26 Na Athalia, mama yake Ahazia, alipoona ya kuwa mwanawe amekufa, akainuka, akawaharibu wazao wote wa kifalme. 2Ila Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu,#11:2 Au, Yoramu. umbu lake Ahazia, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia, akamwiba miongoni mwa hao wana wa mfalme waliouawa, yeye na mlezi wake, na kuwatia katika chumba cha kulala; wakamficha usoni pa Athalia, basi kwa hiyo hakuuawa. 3#2 Nya 22:12; Zab 12:8Alikuwako pamoja naye, amefichwa nyumbani mwa BWANA, miaka sita. Naye Athalia akaitawala nchi.
Yehoyada Apaka Mafuta Mtoto Yoashi
4 # 2 Nya 23:1 Hata mwaka wa saba Yehoyada akatuma, na kuwaleta wakuu wa mamia, wa Wakari, na wa walinzi, akawaleta kwake ndani ya nyumba ya BWANA; akapatana nao, akawaapisha nyumbani mwa BWANA, akawaonyesha huyo mwana wa mfalme. 5#1 Nya 9:25Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoingia siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya mfalme; 6na theluthi mtakuwapo mlangoni pa Suri; na theluthi langoni nyuma ya walinzi; hivyo mtayalinda malinzi ya nyumba, kuzuia watu wasiingie. 7Na sehemu mbili zenu, yaani, wote watokao siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya BWANA kumzunguka mfalme. 8Mtamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake mkononi; naye awaye yote aingiaye ndani ya safu auawe; mkafuatane na mfalme, akitoka na akiingia. 9#2 Nya 23:8Nao wakuu wa mamia wakafanya sawasawa na yote aliyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia sabato, nao watakaotoka sabato, wakaja kwa Yehoyada kuhani.
10 # 1 Sam 21:9; 2 Sam 8:7; 1 Nya 26:26,27; 2 Nya 23:9,10 Naye yule kuhani akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao zilizokuwa za mfalme Daudi, zilizokuwamo nyumbani mwa BWANA. 11Walinzi wakasimama, kila mtu na silaha zake mkononi, kutoka pembe ya kuume ya nyumba mpaka pembe ya kushoto ya nyumba, kando ya madhabahu na nyumba, wakimzunguka mfalme pande zote. 12#Kut 25:16; Kum 17:14; Zab 19:7; 78:5; Isa 8:16; 1 Sam 10:24Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi, wakasema, mfalme na aishi.
Kifo cha Athalia
13 # 2 Nya 23:12 Na Athalia alipoisikia sauti ya walinzi na ya watu, aliingia kwa watu nyumbani kwa BWANA; 14#2 Fal 23:3; 2 Nya 6:13; 34:31; 1 Fal 1:39; Mit 29:2; Mt 21:9; Lk 19:37; Ufu 19:1-7; 1 Fal 18:17,18; 2 Fal 9:23akatazama, na tazama, mfalme amesimama karibu na nguzo kama ilivyokuwa desturi, nao wakuu na wapiga baragumu karibu na mfalme; na watu wote wa nchi wakafurahi, wakapiga baragumu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akalia, Fitina! Fitina! 15Naye Yehoyada kuhani akawaamuru wakuu wa mamia, majemadari wa jeshi, akawaambia, Mtoeni kati ya safu; naye ye yote amfuataye mwueni kwa upanga. Kwani kuhani akasema, Asiuawe nyumbani mwa BWANA. 16#Mwa 9:6; Kut 21:12,14; Law 24:17; Hes 35:30,31; Amu 1:7; 1 Sam 15:33; Mit 11:31; Isa 3:11; Mt 26:52; Yak 2:13; Ufu 13:10Basi wakampisha njia; akaenda kwa njia ya kuingia kwa farasi nyumbani mwa mfalme; akauawa huko.
17 # Kum 5:2,3; 29:1; 2 Fal 23:3; Yer 11:3,6; 1 Sam 10:25; 2 Sam 5:3 Kisha, Yehoyada akafanya mapatano kati ya BWANA na mfalme na watu, ili wawe watu wa BWANA; tena kati ya mfalme na watu. 18#2 Fal 10:26; 2 Nya 23:17,18; Kut 32:20; Kum 7:5; 12:3; Amu 6:25,28; 1 Fal 15:12,13; 2 Nya 23:17Watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunja-vunja kabisa, na Matani kuhani wa Baali wakamwua mbele ya madhabahu. Na Yehoyada kuhani akaweka maakida juu ya nyumba ya BWANA. 19Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa BWANA, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme. 20#Mit 11:10Basi watu wote wa nchi wakafurahi, na mji ukatulia.
Naye Athalia wakamwua kwa upanga karibu na nyumba ya mfalme. 21Yoashi#11:21 Au, Yehoashi. alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala.

Iliyochaguliwa sasa

2 Fal 11: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia