Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Sam 1:17-27

2 Sam 1:17-27 SUV

Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya; (kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema, Wana wa Yuda na wafundishwe haya, Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka! Msiyahubiri mambo haya katika Gathi, Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni; Wasije wakashangilia binti za Wafilisti, Binti za wasiotahiriwa wakasimanga. Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo; Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa, Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta. Kutoka kwa damu yao waliouawa, Kutoka kwa shahamu yao mashujaa, Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, Wala upanga wa Sauli haukurudi bure. Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba. Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu. Jinsi mashujaa walivyoanguka Katikati ya vita! Ee Yonathani, wewe umeuawa Juu ya mahali pako palipoinuka Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake. Jinsi mashujaa walivyoanguka, Na silaha za vita zilivyoangamia!

Soma 2 Sam 1

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Sam 1:17-27