3 Yoh UTANGULIZI
UTANGULIZI
Waraka huu umeandikwa na Yohana ambaye anajiita “Mzee” (tazama utangulizi kwa Waraka wa Kwanza wa Yohana). Ijapokuwa Waraka huu unawekwa kwenye kundi la “Nyaraka kwa Watu Wote” inaonekana kwamba ulitumwa kwa mtu binafsi aitwaye Gayo ambaye alikuwa rafiki yake mwandishi.
Katika Kanisa fulani huko Asia Ndogo alikuwapo kiongozi aliyependa kuchukua madaraka. Huyo anaitwa Diotrefe. Diotrefe alikataa kupokea waalimu na wahubiri halali waliofundisha ukweli wa Injili. Vile vile hakutaka kupokea wajumbe waliotoka kwa mtume Yohana na hivyo kumkataa Mtume Yohana mwenyewe.
Waraka unamtia moyo Gayo aliyekuwa mmoja wa viongozi katika kanisa hilo apokee na kusaidia Wakristo waliosafiri wakihubiri na kufundisha ukweli wa Injili. Anamtahadharisha Gayo kuhusu Diotrefe na kumsifu Demetrio na wengine wanaowapa msaada wahubiri wa kweli.
Iliyochaguliwa sasa
3 Yoh UTANGULIZI: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.