Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mdo 4

4
Petro na Yohana mbele ya Baraza
1 # Lk 22:4,52 Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, 2#Mdo 23:8wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu. 3#Mdo 3:1Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni. 4#Mdo 2:47Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.
5Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu, 6na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu. 7#Mt 21:23Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya? 8#Mt 10:19,20Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, 9kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, 10#Mdo 3:6,13-16jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. 11#Zab 118:22; Mt 21:42Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. 12#Mt 1:21Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
13Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu. 14#Mdo 3:8,9Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. 15Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao, 16#Yn 11:47wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana. 17#Mdo 5:28Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili. 18Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. 19#Mdo 5:29Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; 20maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. 21Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka; 22maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arobaini.
Waumini Waomba wawe na Ujasiri
23Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee. 24#Kut 20:11; Neh 9:6; Zab 146:6; Isa 37:16; Lk 2:29; Ufu 6:10Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; 25#Zab 2:1-2nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako,
Mbona mataifa wamefanya ghasia,
Na makabila wametafakari ubatili?
26Wafalme wa dunia wamejipanga,
Na wakuu wamefanya shauri pamoja
Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.
27 # Mt 27:1-2; Mk 15:1; Lk 23:1,7-11; Yn 18:28-29 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, 28#Mdo 2:23ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. 29#Efe 6:19Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, 30ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. 31#Mdo 2:2,4Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.
Waumini Washiriki Mali zao pamoja
32 # Mdo 2:44-45 Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. 33#Mdo 2:47Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. 34#Mdo 2:45Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, 35wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.
36 # Mdo 11:22,24; 13:4; 15:39 Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, 37alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.

Iliyochaguliwa sasa

Mdo 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia