Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhu 7

7
Ukweli wa Maisha
1 # Mit 22:1; Flp 1:23; Ufu 14:13 Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri;
Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.
2 # Mt 5:4 Heri kuiendea nyumba ya matanga,
Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
3 # 2 Kor 7:10 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko,
Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo.
4Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha.
5Heri kusikia laumu ya wenye hekima,
Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu;
6Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria,
Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu.
Hayo nayo ni ubatili.
7 # Kut 23:8 Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima,
Na rushwa huuharibu ufahamu.
8 # Mit 14:29 Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake,
Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.
9 # Yak 1:19; Mit 16:32 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako,
Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
10Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi?
Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo.
11Hekima ni njema, mfano wa urithi;
Naam, nayo ni bora kwao walionao jua.
12Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo. 13#Isa 14:27Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?
14Siku ya kufanikiwa ufurahi,
Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake.
Mafumbo ya Maisha
15 # Mhu 8:14 Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake.
16 # Mit 25:16; Flp 3:6; Rum 12:3 Usiwe na haki kupita kiasi;
Wala usijiongezee hekima mno;
Kwani kujiangamiza mwenyewe?
17 # Ayu 15:32 Usiwe mwovu kupita kiasi;
Wala usiwe mpumbavu;
Kwani ufe kabla ya wakati wako?
18Ni vizuri kwamba ulishike neno hilo; naam, hata kwa neno hilo tena usiuondoe mkono wako; kwa kuwa mtu yule amchaye Mungu atatoka katika hayo yote.
19Hekima ni nguvu zake mwenye hekima,
Zaidi ya wakuu kumi waliomo mjini.
20 # 1 Fal 8:46; 2 Nya 6:36; Mit 20:9; Rum 3:23; Gal 3:22; 1 Yoh 1:8 Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi. 21Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana. 22Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine.
23Mambo hayo yote mimi nimeyahakikisha katika hekima. Nilisema, Mimi nitakuwa na hekima, lakini imefarakana nami. 24#Kum 30:11-14; Ayu 11:12; Zab 36:6; Isa 55:8,9; Rum 11:33; 1 Tim 6:16Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana, ni mtu yupi awezaye kuyatafuta? 25Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu. 26Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye. 27Tazama, asema Mhubiri, mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili, ili kuitafuta jumla; 28ambayo bado nafsi yangu nikali nikiitafuta, nisiione; mwanamume mmoja katika elfu nimemwona; bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona. 29#Mwa 1:27Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.

Iliyochaguliwa sasa

Mhu 7: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia