Mhu UTANGULIZI
UTANGULIZI
Jina la kitabu hiki latokana na mtu anayejiita kwa lugha ya Kiebrania “Kohelethi”, tafsiri yake ni “Kiongozi”, “Mhutubu wa Mkutano au Kusanyiko”, “Mhubiri” au “Mwalimu wa Hekima”, (1:1; 12; 12:8, 10). Kitabu hiki ni mojawapo wa “Maandiko ya Hekima” (tazama utangulizi wa Agano la Kale). Kwa kuwa Mhubiri asema ni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, hilo ni dokezo kuwa ni mfalme Sulemani (1:1,12,16; 1 Fal 3:12; 4:30-31; 10:7). Lakini mwandishi siye Sulemani bali kufuatana na desturi ya wakati huo aliandika akiwa mtu ajulikanaye sana na alifahamu misemo ya hekima ya Sulemani hata akaandika baadhi yake mnamo karne ya tatu Kabla ya Kristo Kuzaliwa.
Kitabu hiki sio nathari yenye mpangilio, kinachanganya hoja na kurudiarudia mawazo na hoja zilizokwisha elezwa. Mwandishi anazungumzia maana ya maisha kuwa ni bure kabisa (1:2; 12:8) Hata hekima kidunia na maisha yaitwayo ya heri duniani ni ubatili maana mwisho wake ni kifo (2:14,18; 6:1-6; 12:1-7), ni vivyo hivyo kwa kila chenye uhai (3:19-20).
Ujumbe wa Mhubiri ni ubatili wa maisha hapa duniani na kumcha Mungu ni jibu la maisha (12:13). Ijapokuwa kuna mashaka na kukata tamaa mwanadamu hana budi amwamini na kumcha Mungu aliye Muumba na Mtunzaji wa vitu vyote (3:11,14; 9:1; 12:1). Vile vile Mungu atahukumu watu wote wasio mcha (3:17; 8:12-13; 11:9). Kufurahia kazi uitendayo kufuata mapenzi ya Mungu kunatiwa moyo (2:24; 3:13).
Yaliyomo:
1. Maisha ya mtu asiyemcha Mungu ni bure kabisa, Sura 1–6
2. Rai kuhusu ukweli wa maisha, Sura 7–12:8
3. Hatima ya Mhubiri, Sura 12:9-14
Iliyochaguliwa sasa
Mhu UTANGULIZI: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.