Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Efe 5

5
1 # Mt 5:48; Kol 3:12 Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; 2#Kut 29:18; Zab 40:6; Gal 2:20; Ebr 10:10; Kol 3:13; Eze 20:41mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.
Zikataeni Njia za Kipagani
3 # Efe 4:19; Kol 3:5 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; 4#Efe 4:29; Kol 3:8wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. 5#1 Kor 6:9,10; Kol 3:5; Mdo 8:21Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. 6#Rum 1:18; Kol 2:4,8Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. 7Basi msishirikiane nao. 8#Efe 2:11,13; Lk 16:8; 1 Pet 2:9; Yn 12:36Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru, 9kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; 10#Rum 12:2mkihakiki ni nini impendezayo Bwana. 11#Yn 16:8Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; 12#Rum 1:24kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena. 13#Yn 3:20,21Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru. 14#Isa 26:19; 60:1; Rum 13:11; 6:13Hivyo husema,
Amka, wewe usinziaye,
Ufufuke katika wafu,
Na Kristo atakuangaza.
15 # Mt 10:16; Kol 4:5 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16#Kol 4:5mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 17#Rum 12:2Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. 18#Mit 23:31; Lk 21:34Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; 19#Kol 3:16-17; Zab 33:2,3mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; 20#Kol 3:17na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
Nyumba ya Kikristo
21 # 1 Pet 5:5 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.
22 # Kol 3:18; 1 Pet 3:1; Mwa 3:16 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 23#1 Kor 11:3; Kol 1:18Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 # Kol 3:19; 1 Pet 3:7 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26#Tit 3:5ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27#Zab 45:13; 2 Kor 11:2apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. 30#Efe 1:23; 1 Kor 6:15; Mwa 2:23Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. 31#Mwa 2:24Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. 32#Ufu 19:7Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. 33Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.

Iliyochaguliwa sasa

Efe 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia