Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 1

1
1 # Mwa 46:8-27; Kut 6:14 Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo. 2Reubeni, na Simeoni na Lawi, na Yuda; 3na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini; 4na Dani, na Naftali, na Gadi, na Asheri. 5#Mwa 46:26; Kum 10:22Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo. 6#Mwa 50:26; Mdo 7:15; Mhu 1:4Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile. 7#Mdo 7:17; Mwa 46:3; Kum 26:5; Zab 105:24Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.
Waisraeli Wateswa
8 # Mdo 7:18 Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. 9#Zab 105:24Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 10#Mdo 7:19; Zab 10:2; 83:3; Ayu 5:13; Mit 28:16Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. 11#Mwa 15:1; Kut 2:11; 3:7; 5:4; Mit 27:3; Zab 81:6; Mwa 47:11Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 12Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. 13Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 14#Kut 2:23; 22:21; Law 25:14,17; Hes 20:15; Ayu 20:19; Mit 14:31; 22:22; Mdo 7:19,34; Zab 10:17,18; 81:6wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.
15Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; 16akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. 17#Mit 16:6; Dan 3:16,18; 6:13; Mdo 5:29Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume. 18Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai? 19#Yos 2:4; 2 Sam 17:19,20Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia. 20#Mit 11:18; Mhu 8:12; Isa 3:10; Ebr 6:10Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. 21#1 Sam 2:25; 2 Sam 7:11,13,27,29; 1 Fal 2:24; 11:38; Zab 127:1Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba. 22#Mdo 7:19Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.

Iliyochaguliwa sasa

Kut 1: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia