Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 9:1-7

Kut 9:1-7 SUV

Ndipo BWANA akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao, umwambie, BWANA, Mungu wa Waebrania, yuasema, Wape ruhusa watu wangu ili waende wanitumikie. Kwani ukikataa kuwapa ruhusa waende, na kuzidi kuwazuia, tazama, mkono wa BWANA u juu ya wanyama wako wa mifugo walioko kondeni, juu ya farasi, na juu ya punda, na juu ya ngamia, na juu ya ng’ombe, na juu ya kondoo; kutakuwa na tauni nzito sana. Kisha BWANA atawatenga wanyama wa Israeli na wanyama wa Misri; wala hakitakufa kitu cho chote cha wana wa Israeli. Naye BWANA akaweka muda, akasema, Kesho BWANA atalifanya jambo hili katika nchi. BWANA akalifanya jambo hilo siku ya pili, na wanyama wote wa kufugwa wa Misri wakafa; lakini katika wanyama wa wana wa Israeli hakufa hata mmoja. Farao akatuma watu, na tazama, hapana mmoja aliyekufa katika wanyama wa wana wa Israeli. Lakini moyo wa Farao ulikuwa mzito, wala hakuwapa hao watu ruhusa waende zao.