Isa 12
12
Shukrani na Sifa
1 #
Isa 2:11; Zek 14:20,21 Na katika siku hiyo utasema,
Ee BWANA, nitakushukuru wewe;
Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia,
Hasira yako imegeukia mbali,
Nawe unanifariji moyo.
2 #
Kut 15:2; Zab 118:14 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
3 #
Yer 2:13; Yn 4:10,14 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. 4Na katika siku hiyo mtasema,
Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litajeni jina lake kuwa limetukuka.
5Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
6 #
Isa 54:1; Sef 3:14; Lk 19:37-40 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Iliyochaguliwa sasa
Isa 12: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.