Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 55

55
Mwaliko wa Maisha Mema
1 # Yn 4:14; 7:37; 1 Kor 1:22; Mt 13:44; Ufu 21:6; 3:18; 22:17 Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,
Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;
Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,
Bila fedha na bila thamani.
2Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula?
Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha?
Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema,
Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.
3 # Mt 11:28; Isa 54:8; 2 Sam 7:8; Zab 89:28; Mdo 13:34 Tegeni masikio yenu, na kunijia;
Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;
Nami nitafanya nanyi agano la milele,
Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
4 # Mal 3:5; 1 Tim 6:13; Ufu 1:5; Eze 34:23; Dan 9:25; Ebr 2:10 Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu. 5#Isa 52:15; Efe 2:11,12; Mdo 3:13Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.
6 # Zab 32:6; Amo 5:4,14; Mt 5:25; Yn 7:34; 2 Kor 6:2; Ebr 3:13 Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,
Mwiteni, maadamu yu karibu;
7 # Zek 8:17; Yer 3:12 Mtu mbaya na aache njia yake,
Na mtu asiye haki aache mawazo yake;
Na amrudie BWANA,
Naye atamrehemu;
Na arejee kwa Mungu wetu,
Naye atamsamehe kabisa.
8Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. 9Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 10#2 Kor 9:10Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; 11ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
12Maana mtatoka kwa furaha,
Mtaongozwa kwa amani;
Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo;
Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.
13Badala ya michongoma utamea msunobari,
Na badala ya mibigili, mhadesi;
Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina,
Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 55: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia