Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yer 33

33
Kuponywa baada ya Adhabu
1 # Yer 32:2; 37:21 Tena, neno la BWANA likamjia Yeremia mara ya pili, hapo alipokuwa akali amefungwa katika uwanda wa walinzi, kusema, 2#Isa 37:26BWANA alitendaye jambo hili, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake; asema hivi, 3#Mwa 18:17; Kum 4:7,29; Zab 50:15; Isa 55:6,7; Yer 29:12; Mdo 2:21Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. 4#Yer 32:24Maana BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu, na katika habari za nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga; 5Wanakuja kupigana na Wakaldayo, lakini ni kuzijaza kwa mizoga ya watu, niliowaua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, ambao kwa ajili ya uovu wao wote nimeuficha mji huu uso wangu. 6#Yer 30:17Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli. 7#Yer 31:34; Isa 1:26Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza. 8#Zab 85:2,3; Isa 40:2; Yer 31:34; Zek 13:1; Ebr 9:13; Mik 7:18; 1 Yoh 1:7-9Nami nitawasafisha na uovu wao wote, ambao kwa huo wamenitenda dhambi; nami nitawasamehe maovu yao yote, ambayo kwayo wamenitenda dhambi, na kukosa juu yangu. 9#Ezr 1:2; Isa 62:7; 60:5Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo. 10BWANA asema hivi, katika mahali hapo ambapo mnasema kwamba ni ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, naam, katika miji ya Yuda na katika njia za Yerusalemu, zilizo ukiwa, hazina mwanadamu wala mwenyeji wala mnyama, 11#1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 106:1; 107:1; 118:1; 136:1; Ufu 18:23; Law 7:12; Yon 2:9; Ebr 13:15itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema BWANA. 12#Isa 65:10BWANA wa majeshi asema hivi, Katika mahali hapa, palipo ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, na katika miji yake yote, yatakuwapo makao ya wachungaji wakizilaza kondoo zao. 13#Yer 17:26; Law 27:32Katika miji ya nchi ya vilima, katika miji ya nchi tambarare, katika miji ya Negebu, na katika nchi ya Benyamini, na katika mahali palipo karibu na Yerusalemu, na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mikono yake awahesabuye, asema BWANA.
Chipukizi la Haki na Agano la Daudi
14 # Yer 23:5-6; 29:10 Tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapolitimiza neno lile jema nililolinena, katika habari za nyumba ya Israeli, na katika habari za nyumba ya Yuda. 15#Isa 4:2Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii. 16#Kum 33:28; Isa 45:17Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu. 17#2 Sam 7:12-16; 1 Fal 2:4; 1 Nya 17:11-14Maana BWANA asema hivi, Daudi hatakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli; 18#Hes 3:5-10; Mal 1:11; Rum 12:1; 1 Pet 2:5,9; Ufu 1:6wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima. 19Neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema, 20#Mwa 8:22; Zab 89:37; Isa 54:9; Yer 31:36BWANA asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake, 21ndipo agano langu nililolifanya na Daudi, mtumishi wangu, laweza kuvunjika, hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi; tena agano langu nililofanya na Walawi makuhani, wahudumu wangu, laweza kuvunjika. 22#Mwa 13:16; 15:5; Yer 31:37Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa; ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi, mtumishi wangu, na Walawi wanaonihudumia. 23Kisha neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema, 24#Mwa 8:22; Yer 31:35; Zab 74:16; 104:19Je! Hufikiri neno hili walilolisema watu hawa, wakinena, Jamaa zile mbili alizozichagua BWANA amezitupilia mbali? Hivyo ndivyo wanavyowadharau watu wangu, ili wasiwe taifa tena mbele yao. 25BWANA asema hivi, Ikiwa agano langu la mchana na usiku halikai imara, ikiwa mimi sikuziamuru kawaida za mbingu na dunia; 26#Isa 14:1; Yer 31:20; Zek 10:6ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae wazao wake watawale juu ya wazao wa Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu.

Iliyochaguliwa sasa

Yer 33: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia