Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yos 14

14
Mgawanyo wa Nchi ya Magharibi mwa Yordani
1 # Hes 34:17 Kisha hizi ndizo nchi ambazo wana wa Israeli walizitwaa katika nchi ya Kanaani, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na vichwa vya nyumba za mababa wa kabila za Israeli, waliwagawanyia, 2#Hes 26:52-56; 33:54; 34:13; Zab 16:5; Mit 16:33; 18:18kwa kuandama hiyo kura ya urithi wao, vile vile kama BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa, kwa ajili ya hizo kabila kenda, na hiyo nusu ya kabila. 3#Hes 32:33; 34:14-15; Kum 3:12-17; Yos 13:8Kwa kuwa Musa alikuwa amekwisha kuwapa urithi hizo kabila mbili na nusu, ng’ambo ya pili ya Yordani; lakini hakuwapa Walawi urithi uwao wote kati yao. 4#Mwa 48:5; 1 Nya 5:1,2Kwa kuwa wana wa Yusufu walikuwa kabila mbili, Manase na Efraimu; nao hawakuwapa Walawi sehemu katika hiyo nchi, isipokuwa waliwapa miji wapate kuikaa, pamoja na viunga vyake kwa ajili ya wanyama wao wa mifugo, na kwa ajili ya riziki zao. 5#Hes 35:2; Yos 21:2; Eze 45:1-8; 48:8,22Vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa, hao wana wa Israeli walifanya vivyo, nao wakaigawanya hiyo nchi.
Kalebu Agawiwa Hebroni
6 # Hes 14:24,30; 32:8,12; 13:26; Yos 15:17; Kum 1:19,36 Wakati huo wana wa Yuda walimkaribia Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno BWANA alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea. 7#Hes 13:1-30Mimi nilikuwa mtu wa miaka arobaini umri wangu, hapo Musa mtumishi wa BWANA aliponituma niende kutoka Kadesh-barnea ili kuipeleleza hiyo nchi; nami nilimletea habari tena, kama ilivyokuwa ndani ya moyo wangu. 8#Hes 14:24; Kum 1:36; Ufu 14:4Lakini wale ndugu zangu waliokwea kwenda pamoja nami waliiyeyusha mioyo ya watu; ila mimi nilimfuata BWANA, Mungu wangu, kwa utimilifu. 9#Hes 14:24; 13:22; Yos 1:3Kisha Musa akaniapia siku hiyo, akasema, Hakika hiyo nchi ambayo miguu yako imekanyaga itakuwa ni urithi kwako wewe, na kwa watoto wako milele, kwa sababu wewe umemfuata BWANA, Mungu wako, kwa utimilifu. 10#Hes 14:30; Kum 31:2; Zab 90:10Sasa basi, angalia, yeye BWANA ameniweka hai, kama alivyosema, miaka hii arobaini na mitano, tangu wakati huo BWANA alipomwambia Musa neno hilo, wakati Israeli waliokuwa wakienenda barani; na sasa tazama, hivi leo nimepata miaka themanini na mitano umri wangu. 11#Kum 34:7; 31:2Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kutoka nje na kuingia ndani. 12#Hes 21:34; 1 Sam 14:6; 2 Nya 14:11,12; Zab 18:32; 44:3; Rum 8:31; Flp 4:13; Yos 15:14; Amu 1:10Basi sasa unipe mlima huu, ambao BWANA alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye BWANA atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama BWANA alivyonena. 13#Amu 1:20; Mwa 47:7-10; Yos 22:6; 10:37; 21:11; 1 Nya 6:55Yoshua akambarikia, akampa Kalebu, huyo mwana wa Yefune, Hebroni kuwa urithi wake. 14Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi, hata leo; kwa sababu alimwandama BWANA, Mungu wa Israeli, kwa utimilifu. 15#Mwa 23:2; Yos 15:13; 11:23Basi jina la Hebroni hapo kwanza uliitwa Kiriath-arba; huyo Arba alikuwa ni mtu mkubwa kupita wenziwe wote katika hao Waanaki. Hiyo nchi nayo ikatulia, vita vikakoma.

Iliyochaguliwa sasa

Yos 14: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia