Lk 3:21-38
Lk 3:21-38 SUV
Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe. Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli, wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu, wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai, wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, wa Yuda, wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri, wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri, wa Yoshua, wa Eliezeri, wa Yorimu, wa Mathati, wa Lawi, wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu, wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, wa Daudi, wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nashoni, wa Aminadabu, wa Aramu, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda, wa Yakobo, wa Isaka, wa Ibrahimu, wa Tera, wa Nahori, wa Serugi, wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala, wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki, wa Methusela, wa Henoko, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani, wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.