Mt 15
15
Mapokeo ya Wazee
1 #
Mk 7:1-23
Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema, 2#Kum 4:2; Lk 11:38Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. 3Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? 4#Kut 20:12; 21:17; Kum 5:16; Law 20:9Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. 5Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, 6basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu. 7#Isa 29:13Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
8 #
Isa 29:13
Watu hawa huniheshimu kwa midomo;
Ila mioyo yao iko mbali nami.
9Nao waniabudu bure,
Wakifundisha mafundisho
Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Mambo Yatiayo Unajisi
10Akawaita makutano akawaambia 11#Mt 12:34; 1 Tim 4:4Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi. 12Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa? 13#Yn 15:2Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa. 14#Lk 6:39; Mt 23:24; Yn 9:40; Rum 2:19Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili. 15Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo. 16Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili? 17Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? 18#Mt 12:34Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. 19#Mwa 8:21Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; 20hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.
Imani ya Mwanamke Mkanaani
21 #
Mk 7:24-30
Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. 22Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. 23Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. 24#Mt 10:6Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 25Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie. 26Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. 27Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. 28#Mt 8:10,13Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
Yesu Awaponya Watu Wengi
29 #
Mk 7:31
Yesu akaondoka huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko. 30Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya; 31#Mk 7:37hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.
Kulishwa kwa Watu Elfu Nne
32 #
Mk 8:1-10
#
Mt 14:14
Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula, tena kuwaaga wakifunga sipendi, wasije wakazimia njiani. 33Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii? 34Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache. 35Akawaagiza mkutano waketi chini; 36akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano. 37Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa. 38Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto. 39Akawaaga makutano, akapanda chomboni, akaenda pande za Magadani.
Iliyochaguliwa sasa
Mt 15: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.