Mt 18
18
Ukuu wa Kweli
1 #
Lk 22:24
#
Mk 9:33-47; Lk 9:46-48 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema, 2Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, 3#Mk 10:15; Lk 18:17; Mt 19:14; Yn 3:3-5akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Majaribu ya Dhambi
4Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. 5#Mt 10:40; Yn 13:20Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi; 6#Lk 17:1,2bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari. 7Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha! 8#Mt 5:29,30Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. 9#Mt 5:29Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.
Mfano wa Kondoo Aliyepotea
10 #
Ebr 1:14
Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. 11#Lk 19:10[Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.] 12#Lk 15:4-7Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? 13Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea. 14Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.
Kumwonya Anayekukosea
15 #
Lk 17:3; Law 19:17; Gal 6:1 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16#Kum 19:15La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. 17#1 Kor 5:13Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. 18#Mt 16:19; Yn 20:23Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. 19#Mk 11:24Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20#Mt 28:20; Yn 14:23Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Kusameheana
21 #
Lk 17:3-4
Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? 22Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
Mfano wa Mtumishi Asiyesamehe
23Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. 24Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta#18:24 Talanta moja ni kama shilingi 5,000. elfu kumi. 25Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. 26Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 27Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. 28Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari#18:28 Dinari moja ni kama senti 75. mia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho. 29Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 30Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. 31Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. 32Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? 34#Mt 5:26Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. 35#Mt 6:14,15Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.
Iliyochaguliwa sasa
Mt 18: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.