Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 31

31
Vita Dhidi ya Midiani
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Hes 25:17; Kum 32:35,43; Zab 94:1; Mwa 15:15; 25:8; 35:29; Hes 27:13Walipize kisasi wana wa Israeli juu ya Wamidiani; kisha baadaye utakusanywa uwe pamoja na watu wako. 3#Kum 32:35; Yer 50:28; Zab 94:1; Rum 12:19; Ebr 10:30Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipiza kisasi BWANA, juu ya Midiani. 4Katika kila kabila mtatoa watu elfu, katika kabila zote za Israeli, nanyi mtawapeleka waende vitani. 5Basi walitolewa katika maelfu ya Israeli, elfu moja ya kila kabila, watu waume kumi na mbili elfu walioandaliwa kwa vita. 6#Hes 10:9Basi Musa akawapeleka, watu elfu wa kila kabila waende vitani, wao na Finehasi mwana wa Eleazari kuhani, waende vitani, na vile vyombo vya mahali patakatifu, na hizo tarumbeta za kupiga sauti za kugutusha mkononi mwake. 7#Kum 20:13; Amu 21:11; 1 Sam 27:9; 1 Fal 11:15,16; Amu 6:1,2,33Nao wakapigana na Midiani kama BWANA alivyomwagiza Musa; nao wakamwua kila mume. 8#Yos 13:21; Hes 22:10; 24:25; Yos 13:22; Zab 9:12; Yud 1:11; Ufu 2:14; 19:20Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga. 9Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng’ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara. 10Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na marago yao yote wakayateketeza kwa moto. 11#Kum 20:14Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama. 12Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
Kurejea Toka Vitani
13Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya marago. 14Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao maakida wa elfu elfu, na wakuu wa mia mia, hao waliorudi kutoka katika kupiga vita. 15#Kum 2:34; 20:13; Yos 6:21; 8:25; 10:40; 11:14; 1 Sam 15:3Musa akawauliza, Je! Mmewaponya wanawake wote hai? 16#Hes 25:1-9; 24:14; Yos 22:17; Zab 106:28,29; Hos 9:10; Mik 6:5; 2 Pet 2:15; Ufu 2:14Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie BWANA dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa BWANA. 17#Amu 21:11Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye. 18Lakini hao watoto wote wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye, mtawaweka hai kwa ajili yenu. 19#Hes 5:2; 19:11; 9:6,10Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya marago muda wa siku saba; mtu awaye yote aliyemwua mtu, na awaye yote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu. 20Na katika habari ya kila nguo, na kila kitu kilichofanywa cha ngozi, na kazi yote ya singa za mbuzi, na vyombo vyote vilivyofanywa vya mti, mtajitakasa wenyewe; 21Kisha Eleazari kuhani akawaambia waume wa vita wote waliokwenda vitani, Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyomwagiza Musa; 22lakini dhahabu, na fedha, na shaba, na chuma, na bati, na risasi, 23#Hes 8:7; 19:9,17kila kitu kiwezacho kuuhimili moto, mtakipitisha katika moto, nacho kitakuwa safi, pamoja na haya kitatakaswa kwa hayo maji ya farakano; na kila kitu kisichouhimili moto mtakipitisha katika hayo maji. 24#Law 11:25; 14:9; Hes 19:10,22; Zab 51:2; Zek 13:1; Efe 5:26; Ebr 9:9,10; 10:22; 1 Yoh 1:7Nanyi mtazifua nguo zenu siku ya saba, nanyi mtakuwa safi, kisha baadaye mtaingia maragoni.
Mgawanyo wa Mateka na Nyara
25Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 26Fanya jumla ya hayo mateka ya wanadamu, na ya wanyama pia, wewe, na Eleazari kuhani, na wakuu wa nyumba za baba za mkutano; 27#Yos 22:8; 1 Sam 30:4; Zab 68:12ukagawanye nyara mafungu mawili; kati ya watu waliozoea vita, waliotoka nje waende vitani, na huo mkutano wote; 28#2 Sam 8:11; 1 Nya 18:11; 26:27; Isa 18:7; 23:18; Mt 22:21; Hes 18:26kisha uwatoze hao watu wa vita waliotoka kwenda vitani sehemu kwa ajili ya BWANA; mmoja katika mia tano, katika wanadamu, na katika ng’ombe, na katika punda, na katika kondoo; 29twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA. 30#Hes 3:7,8; 18:3,4; 1 Nya 9:27-29; 23:32Na katika hiyo nusu ya wana wa Israeli utatwaa mmoja atakayetolewa katika kila hamsini, katika wanadamu, na katika ng’ombe, na katika punda, na katika kondoo, maana, katika wanyama wote, ukawape Walawi, hao walindao ulinzi wa maskani ya BWANA. 31Musa na Eleazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa. 32Basi masazo ya hizo nyara walizotwaa watu wa vita, zilikuwa ni kondoo mia sita na sabini na tano elfu, 33na ng’ombe sabini na mbili elfu, 34na punda sitini na moja elfu, 35tena wanadamu jumla yao ilikuwa thelathini na mbili elfu, katika hao wanawake ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye. 36Na hiyo nusu ambayo ilikuwa ni sehemu ya hao waliotoka kwenda vitani, hesabu yake ilikuwa kondoo mia tatu na thelathini na saba elfu na mia tano; 37#Law 25:23; Kum 10:14; Zab 24:1; 50:12; Mit 3:9; Mt 22:21; Mk 12:17; Lk 20:25; 1 Kor 10:26,28na kodi ya BWANA katika hao kondoo ilikuwa kondoo mia sita na sabini na watano. 38Tena, ng’ombe walikuwa thelathini na sita elfu; na katika hao kodi ya BWANA ilikuwa ng’ombe sabini na wawili. 39Na punda walikuwa thelathini elfuna mia tano, katika hao kodi ya BWANA ilikuwa punda sitini na mmoja. 40Na wanadamu walikuwa watu kumi na sita elfu; katika hao sehemu ya BWANA ilikuwa ni watu thelathini na wawili. 41#Hes 5:9,10; 18:8,19Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa. 42Tena katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, ambayo Musa aliitenga na watu waliokwenda vitani, 43(basi hiyo nusu ya mkutano ilikuwa ni kondoo mia tatu na thelathini na saba elfu na mia tano, 44na ng’ombe thelathini na sita elfu, 45na punda thelathini elfu, na mia tano, 46na wanadamu kumi na sita elfu;) 47na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, waliolinda ulinzi wa maskani ya BWANA; kama BWANA alivyomwagiza Musa. 48Na majemadari waliokuwa juu ya elfu elfu za hiyo jeshi, na maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, wakamkaribia Musa; 49#Kut 23:7; Law 26:7-9; Zab 72:14; 116:15; 1 Sam 30:19wakamwambia Musa wakisema, Sisi watumishi wako tumefanya jumla ya hesabu ya watu wa vita walio chini ya mikono yetu, na hapana hata mmoja aliyetupungukia. 50#Kut 30:12,16; Law 17:11; Mt 20:28; Rum 3:25Nasi tumeleta matoleo ya BWANA, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za muhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya BWANA. 51Musa na Eleazari kuhani wakapokea kwao hiyo dhahabu, maana, vile vyombo vyote vilivyofanyizwa. 52Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa BWANA, ya maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, ilikuwa shekeli kumi na sita elfu na mia saba na hamsini. 53#Kum 20:14(Kwa kuwa hao watu wa vita walikuwa wametwaa nyara, kila mtu nafsi yake.) 54#Hes 16:40; Kut 30:16; Yos 4:7; Zek 6:14; Lk 22:19; Mdo 10:4Basi Musa na Eleazari kuhani wakapokea hiyo dhahabu mikononi mwa hao maakida wa elfu elfu na wa mia mia, na kuileta ndani ya hema ya kukutania, ili iwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 31: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia