Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 32

32
Ushindi na Mgawanyo wa Kanaani
1 # Hes 21:32; Yos 13:25; 2 Sam 24:5; Isa 16:8,9 Basi wana wa Reubeni, na hao wana wa Gadi, walikuwa na wanyama wa mifugo wengi sana; nao walipoona nchi ya Yazeri, na nchi ya Gileadi, ya kuwa mahali hapo palikuwa ni mahali pa kuwafaa wanyama; 2hao wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakamwendea Musa na Eleazari kuhani, na wakuu wa mkutano, wakanena nao, wakisema, 3Atarothi, na Diboni, na Yazeri, na Nimra, na Heshboni, na Eleale, na Sebamu, na Nebo na Beoni, 4#Hes 21:24,34nchi hiyo ambayo BWANA aliipiga mbele ya mkutano wa Israeli, ni nchi ifaayo kwa mfugo wa wanyama, nasi watumishi wako tuna wanyama. 5Wakasema, Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, sisi watumishi wako na tupewe nchi hii iwe milki yetu; usituvushe mto wa Yordani. 6Musa akawaambia wana wa Gadi na wana wa Reubeni, Je! Ndugu zenu waende vitani nanyi mtaketi hapa? 7Mbona mwawavunja mioyo yao wana wa Israeli, wasivuke na kuingia nchi hiyo ambayo BWANA amewapa? 8#Hes 13:3,17-33; Kum 1:22Ndivyo walivyofanya baba zenu, hapo nilipowatuma kutoka Kadesh-barnea ili waende kuiangalia hiyo nchi. 9#Hes 1:10; 13:24,31; Kum 1:24Kwa kuwa walipokwea na kuingia bonde la Eshkoli, na kuiona nchi, wakawavunja mioyo wana wa Israeli, ili wasikwee kuingia nchi BWANA aliyowapa. 10#Hes 14:11; Kum 1:34; Zab 95:11; Eze 20:15; Ebr 3:8-19Na siku ile hasira za BWANA ziliwaka, naye akaapa, akisema, 11#Kum 1:35; Hes 14:24Hakika yangu hapana mtu mmoja katika wale watu waliotoka Misri, tangu huyo aliyepata umri wa miaka ishirini, na zaidi, atakayeiona hiyo nchi niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; kwa sababu hawakuniandama kwa moyo wote; 12#Kum 1:36; Yos 14:8,9; Ayu 4:7; Zab 37:29; Mit 11:31ila Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni; kwa kuwa wao wamemwandama BWANA kwa moyo wote. 13#Hes 14:33; 26:64Na hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huku jangwani muda wa miaka arobaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa BWANA kikaisha angamia. 14#Kum 1:34Na tazama, ninyi mmeinuka badala ya baba zenu, maongeo ya watu wenye dhambi, ili kuongeza tena hizo hasira kali za BWANA juu ya Israeli. 15#Kum 30:17; Yos 22:16,18; 2 Nya 7:19; 15:2Kwa kuwa mkigeuka msimwandame, yeye atawaacha tena nyikani; nanyi mtawaangamiza watu hawa wote. 16Basi wakamwendea karibu, na kusema, Sisi tutafanya mazizi hapa kwa ajili ya wanyama wetu wa mifugo, na kujenga miji kwa ajili ya watoto wetu; 17#Yos 4:12,13lakini sisi wenyewe tutakuwa tayari na silaha zetu kutangulia mbele ya wana wa Israeli, hata tutakapowafikisha mahali pao; na watoto wetu watakaa katika hiyo miji yenye maboma, kwa sababu ya wenyeji wa nchi. 18#Yos 22:4Sisi hatutarudia nyumba zetu, hata wana wa Israeli watakapokuwa wamekwisha kurithi kila mtu urithi wake. 19#Yos 12:1; 13:8Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng’ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa Yordani kwa mashariki. 20#Kum 3:18; Yos 1:14; 4:12,13Basi Musa akawaambia, Kama mtafanya jambo hili; kama mtajivika silaha, ili kutangulia mbele ya BWANA mwende vitani, 21tena kama kila mume wa kwenu mwenye kuchukua silaha atavuka Yordani mbele ya BWANA, hata atakapokuwa amekwisha watoa adui zake mbele yake, 22#Kum 3:20; Yos 11:23; 18:1; 22:4,9; Kum 3:12; Yos 1:15; 13:8,32na hiyo nchi kushindwa mbele za BWANA; ndipo baadaye mtarudi, nanyi mtakuwa hamna hatia mbele za BWANA, wala kwa Israeli; na nchi hii itakuwa milki yenu mbele za BWANA. 23#Mwa 4:7; 44:16; Zab 140:11; Mit 13:21; Isa 3:11; 59:12; Rum 2:9; 1 Kor 4:5Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata hapana budi. 24#Hes 32:16,34Basi, jengeni miji kwa ajili ya watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; mkayafanye hayo mliotamka kwa vinywa vyenu. 25Ndipo wana wa Gadi na wana wa Reubeni wakanena na Musa, na kumwambia, Sisi watumishi wako tutafanya kama wewe bwana wangu utuagizavyo. 26#Yos 1:14Watoto wetu, na wake wetu, na kondoo zetu, na ng’ombe zetu wote, watakuwa hapo katika miji ya Gileadi; 27#Yos 4:12lakini sisi watumishi wako tutavuka, kila mume aliyevaa silaha za vita, mbele za BWANA, tuende vitani, kama wewe bwana wangu usemavyo.
28 # Yos 1:12-15 Basi Musa akamwagiza Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na wakuu wa nyumba za mababa za kabila za wana wa Israeli, katika habari za watu hao. 29Musa akawaambia, Kwamba wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, watavuka Yordani pamoja nanyi, kila mtu aliyevaa silaha kwa vita, mbele za BWANA, nayo nchi itashindwa mbele yenu; ndipo mtawapa nchi ya Gileadi kuwa milki yao; 30lakini ikiwa hawataki kuvuka pamoja nanyi, hali wamevaa silaha zao, ndipo watakuwa na milki zao kati yenu katika nchi ya Kanaani. 31Wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakajibu na kusema, Kama BWANA alivyotuambia sisi watumishi wako, ndivyo tutakavyofanya. 32Tutavuka, hali tumevaa silaha zetu, mbele za BWANA, kuingia nchi ya Kanaani, nayo milki ya urithi wetu itakuwa ng’ambo ya pili ya Yordani. 33#Kum 3:12; Yos 12:6; 13:8; 22:4; Hes 21:24; Kum 2:30-35; 3:1-8; Zab 135:10,11; 136:18Basi Musa akawapa wao, maana, wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, mwana wa Yusufu, ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, hiyo nchi, kama miji yao ilivyokuwa, pamoja na mipaka yake, maana, miji ya hiyo nchi iliyozunguka kotekote. 34#Hes 33:45; Kum 2:36Kisha wana wa Gadi wakajenga Diboni, na Atarothi, na Aroeri; 35na Atrothi-shofani, na Yazeri, na Yogbeha; 36na, Beth-nimra, na Beth-harani; miji yenye maboma, na mazizi ya kondoo. 37Na wana wa Reubeni wakajenga Heshboni, na Eleale, na Kiriathaimu; 38#Isa 46:1; Hes 22:41; Kut 23:13na Nebo, na Baal-meoni, (majina yake yalikuwa yamegeuzwa) na Sibma; nao wakaiita miji waliyoijenga majina mengine. 39#Mwa 50:23; Hes 26:29; Yos 17:1Na wana wa Makiri mwana wa Manase wakaenda Gileadi, na kuitwaa, na kuwapokonya Waamori waliokuwamo humo. 40#Kum 3:12; Yos 17:1Basi Musa akampa Makiri, mwana wa Manase, Gileadi, naye akakaa humo. 41#Kum 3:14; Yos 13:30; 1 Nya 2:21; Amu 10:4; 1 Fal 4:13Kisha Yairi mwana wa Manase akaenda na kuvitwaa vijiji vya Gileadi. Akaviita jina lake Hawoth-yairi. 42#2 Sam 18:18; Zab 49:11Kisha Noba akaenda na kutwaa Kenathi na vijiji vyake, na kuita jina lake Noba, kwa kuandama jina lake mwenyewe.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 32: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia