Flm UTANGULIZI
UTANGULIZI
Waraka huu wa Paulo kwa rafiki yake Filemoni (1:17) una nafasi ya pekee katika Nyaraka zote za Agano Jipya. Ni Waraka mfupi kuliko Nyaraka zote za Paulo na, tofauti na Nyaraka zake nyingine, huu ni wa binafsi kabisa. Mlengwa wa Waraka huu ni mtu aitwaye Filemoni. Kwa kuwa Onesimo, mtumwa wa Filemoni, anatajwa mahali pengine kama mwenyeji wa Kolosai (Kol 4:9) kama vile Arkipo ambaye anatajwa katika sehemu ya salamu ya Waraka huu (aya 2), wengi wanafikiri kwamba Filemoni naye pia alikuwa mwenyeji wa Kolosai. Lakini wengine wanafikiri alitoka Efeso. Filemoni alikuwa mtu maarufu na mkarimu ambaye labda alipata kuwa mkristo kwa njia ya Paulo (aya 19) na kanisa lilikutana nyumbani kwake (aya 2).
Kwa kuwa Paulo aliwajua vizuri Filemoni na Onesimo aliandika Waraka huu ili kumsihi Filemoni ampokee tena mtumwa wake yaani Onesimo. Paulo anamwomba ampokee sio kama mtumwa aliyetoroka tu bali ndugu katika Kristo.
Waraka huu kwa Filemoni unaonyesha jinsi Paulo alivyoweza kutumia hali mpya ya Kikristo kukabili hali ya utumwa wa mtu kwa mtu mwingine wakati kimsingi hakuna mtu aliye mtumwa wa mtu mwingine na kwamba Wakristo ni ndugu katika kuungana na Bwana. Paulo anatarajia kwamba Filemoni atampokea huyo mtumwa wake mtoro kwa njia inayoonyesha maisha mapya ya Kikristo, tena Paulo yuko tayari kulipa chochote ambacho Onesimo alikuwa amechukua kutoka kwa Filemoni.
Iliyochaguliwa sasa
Flm UTANGULIZI: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.