Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Flp 2

2
Kuiga Unyenyekevu wa Kristo
1Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, 2ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. 3#Gal 5:26; Rum 12:10Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. 4#1 Kor 10:24,33Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. 5Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6#Yn 1:1,2; 17:5; Mwa 1:27; 3:5ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7#Isa 53:3; 2 Kor 8:9; Ebr 2:14,17bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8#Ebr 12:2; 5:8; Yn 10:17tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9#Mdo 2:33; Efe 1:21; Ebr 1:3,4Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10#Isa 45:23; Yn 5:23; Ufu 5:13ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Kuangaza kama Mianga Ulimwenguni
12 # 1 Pet 1:17; Zab 2:11 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. 13#Yn 15:5; 2 Kor 3:5; 1 The 2:13Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
14 # 1 Pet 4:9 Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, 15#Kum 32:5; Mt 5:14; 10:16; Flp 1:10; Efe 5:8; Kum 32:5; Mdo 2:40mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, 16#1 The 2:19; Gal 2:2; Isa 49:4; 65:23mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure. 17#Rum 15:16; 2 Tim 4:6Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote. 18#Flp 3:1; 4:4Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami.
Timotheo na Epafrodito
19Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. 20#1 Kor 16:10Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. 21#2 Tim 4:10,16; Gal 4:17Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu. 22Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake. 23Basi, natumaini kumtuma huyo mara, hapo nitakapojua yatakayonipata. 24#Flp 1:25Nami naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe hivi karibu.
25 # Flp 4:18 Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu. 26Kwa kuwa alikuwa na shauku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi. 27Kwa maana alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni. 28Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma, ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu. 29#1 Kor 16:16; 1 Tim 5:17Mpokeeni, basi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa. 30Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akaponza roho yake; ili kusudi ayatimize yaliyopungua katika huduma yenu kwangu.

Iliyochaguliwa sasa

Flp 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia