Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 11

11
1Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA;
Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.
2 # Dan 4:30 Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu;
Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.
3Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza
Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
4 # Eze 7:19; Sef 1:18; Mwa 7:1 Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu;
Bali haki huokoa na mauti.
5Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake;
Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.
6 # 1 Tim 4:8; Mhu 10:8 Haki yao wenye haki itawaokoa;
Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
7Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea;
Na matumaini ya uovu huangamia.
8Mwenye haki huokolewa katika dhiki,
Na mtu mwovu ataiingia badala yake.
9 # Ayu 8:13 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake;
Bali wenye haki watapona kwa maarifa.
10 # Est 8:15 Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi;
Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.
11Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki;
Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.
12Asiye na akili humdharau mwenziwe;
Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
13Mwenye kitango akisingizia hufunua siri;
Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
14 # 1 Fal 12:1 Pasipo mashauri taifa huanguka;
Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
15Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;
Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.
16Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima;
Na watu wakali hushika mali siku zote.
17 # Mt 25:34 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake;
Aliye mkali hujisumbua mwili wake.
18 # Hos 10:12; Gal 6:8,9 Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu;
Apandaye haki ana thawabu ya hakika.
19Haki huelekea uzima;
Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe.
20Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA;
Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza.
21Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu;
Bali wazao wa wenye haki wataokoka.
22Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe,
Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.
23 # Rum 2:8 Haja ya mwenye haki ni mema tu;
Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu.
24Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi;
Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
25 # Mt 5:7 Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa;
Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.
26 # Amo 8:5; Ayu 29:13 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani;
Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake.
27 # Est 7:10 Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili;
Atafutaye madhara, hayo yatamjia.
28 # Mk 10:24; Lk 12:21; 1 Tim 6:17; Yer 17:8 Azitegemeaye mali zake ataanguka;
Mwenye haki atasitawi kama jani.
29 # Mhu 5:16 Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo;
Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.
30Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima;
Na mwenye hekima huvuta roho za watu.
31 # 1 Pet 4:18; Yer 25:29 Tazama, mwenye haki atalipwa duniani;
Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi?

Iliyochaguliwa sasa

Mit 11: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia