Mit 28:6-12
Mit 28:6-12 SUV
Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri. Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima; Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye. Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema. Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe; Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana. Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha.