Zab 113
113
Mungu Msaidizi wa Mhitaji
1Haleluya.
Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,
Lisifuni jina la BWANA.
2 #
Dan 2:20
Jina la BWANA lihimidiwe
Tangu leo na hata milele.
3 #
Isa 59:19; Hab 2:14; Mal 1:11; Ufu 11:15 Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la BWANA husifiwa.
4BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5Ni nani aliye mfano wa BWANA,
Mungu wetu aketiye juu;
6 #
Isa 57:15
Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani?
7 #
1 Sam 2:8; Isa 26:19; Dan 12:2 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8 #
Ayu 36:7
Amketishe pamoja na wakuu,
Pamoja na wakuu wa watu wake.
9 #
1 Sam 2:5; Gal 4:27 Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa,
Awe mama ya watoto mwenye furaha.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 113: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.