Zab 135
135
Sifa kwa Wema na Ukuu wa Mungu
1Haleluya.
Lisifuni jina la BWANA,
Enyi watumishi wa BWANA, sifuni.
2 #
Lk 2:37
Ninyi msimamao nyumbani mwa BWANA,
Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu.
3Msifuni BWANA kwa kuwa BWANA ni mwema,
Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza.
4 #
Kut 19:5; Kum 7:6,7 Kwa sababu BWANA amejichagulia Yakobo,
Na Israeli, wawe watu wake hasa.
5Maana najua mimi ya kuwa BWANA ni mkuu,
Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote.
6BWANA amefanya kila lililompendeza,
Katika mbingu na katika nchi,
Katika bahari na katika vilindi vyote.
7 #
Mwa 2:6; Ayu 5:10; Yer 10:13; Zek 10:1; Ayu 28:25; 38:22 Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi;
Huifanyia mvua umeme;
Hutoa upepo katika hazina zake.
8Aliwapiga wazaliwa wa kwanza wa Misri,
Wa wanadamu na wa wanyama.
9Alipeleka ishara na maajabu kati yako, Ee Misri,
Juu ya Farao na watumishi wake wote.
10 #
Hes 21:24
Aliwapiga mataifa mengi,
Akawaua wafalme wenye nguvu;
11 #
Yos 12:7
Sihoni, mfalme wa Waamori,
Na Ogu, mfalme wa Bashani,
Na falme zote za Kanaani.
12 #
Mwa 17:8
Akaitoa nchi yao iwe urithi,
Urithi wa Israeli watu wake.
13 #
Kut 3:15
Ee BWANA, jina lako ni la milele,
BWANA, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.
14 #
Kum 32:36
Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake,
Atawahurumia watumishi wake.
15 #
Zab 115:4-8; Ufu 9:20 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,
Kazi ya mikono ya wanadamu.
16Zina vinywa lakini hazisemi,
Zina macho lakini hazioni,
17Zina masikio lakini hazisikii,
Wala hamna pumzi vinywani mwake.
18Wazifanyao watafanana nazo,
Na kila mmoja anayezitumainia.
19Enyi mlango wa Israeli, mhimidini BWANA;
Enyi mlango wa Haruni, mhimidini BWANA;
20Enyi mlango wa Lawi, mhimidini BWANA;
Ninyi mnaomcha BWANA, mhimidini BWANA.
21Na ahimidiwe BWANA toka Sayuni,
Akaaye Yerusalemu.
Haleluya.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 135: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.