Zab 148
148
Sifa kwa Utukufu Mkuu wa Mungu
1Haleluya.
Msifuni BWANA kutoka mbinguni;
Msifuni katika mahali palipo juu.
2 #
Dan 7:10; Ebr 1:7 Msifuni, enyi malaika wake wote;
Msifuni, majeshi yake yote.
3Msifuni, jua na mwezi;
Msifuni, nyota zote zenye mwanga.
4 #
1 Fal 8:27
Msifuni, enyi mbingu za mbingu,
Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.
5 #
Ebr 11:3
Na vilisifu jina la BWANA,
Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.
6 #
Yer 33:25
Amevithibitisha hata milele na milele,
Ametoa amri wala haitapita.
7 #
Isa 43:20
Msifuni BWANA kutoka nchi,
Enyi nyangumi na vilindi vyote.
8Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke,
Upepo wa dhoruba ulitendao neno lake.
9 #
Isa 49:13
Milima na vilima vyote,
Miti yenye matunda na mierezi yote.
10Hayawani, na wanyama wafugwao,
Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.
11 #
Mdo 17:28
Wafalme wa dunia, na watu wote,
Wakuu, na makadhi wote wa dunia.
12Vijana waume, na wanawali,
Wazee, na watoto;
13 #
Isa 6:3; Flp 2:9 Na walisifu jina la BWANA,
Maana jina lake peke yake limetukuka;
Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
14 #
Efe 2:17; 1 Pet 2:9 Naye amewainulia watu wake pembe,
Sifa za watauwa wake wote;
Wana wa Israeli, watu walio karibu naye.
Haleluya.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 148: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.