Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 29

29
Sauti ya Mungu katika Dhoruba
Zaburi ya Daudi.
1 # Zab 96:7-9; 1 Nya 16:28,29 Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu;
2Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.
3Sauti ya BWANA i juu ya maji;
Mungu wa utukufu alipiga radi;
BWANA yu juu ya maji mengi.
4Sauti ya BWANA ina nguvu;
Sauti ya BWANA ina adhama;
5Sauti ya BWANA yaivunja mierezi;
Naam, BWANA aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni;
6 # Zab 114:4; Kum 3:9 Airusha-rusha kama ndama wa ng’ombe;
Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati.
7Sauti ya BWANA yaipasua miali ya moto;
8 # Hes 13:26 Sauti ya BWANA yalitetemesha jangwa;
BWANA alitetemesha jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya BWANA yawazalisha ayala,
Na kuifichua misitu;
Na ndani ya hekalu lake
Wanasema wote, Utukufu.
10 # Zab 93:4 BWANA aliketi juu ya Gharika;
Naam, BWANA ameketi hali ya mfalme milele.
11 # Isa 40:29 BWANA atawapa watu wake nguvu;
BWANA atawabariki watu wake kwa amani.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 29: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia