Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 32

32
Shangwe kwa Kusamehewa
Ya Daudi. Funzo
1 # Rum 4:7-8; Zab 85:2 Heri aliyesamehewa dhambi,
Na kusitiriwa makosa yake.
2 # Law 17:4; Rum 5:13; Yn 1:47; 2 Kor 1:12 Heri BWANA asiyemhesabia upotovu,
Ambaye rohoni mwake hamna hila.
3Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa
Kwa kuugua kwangu mchana kutwa.
4Kwa maana mchana na usiku
Mkono wako ulinilemea.
Jasho langu likakauka hata nikawa
Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
5 # Mit 28:13; Isa 65:24; Lk 15:18 Nalikujulisha dhambi yangu,
Wala sikuuficha upotovu wangu.
Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,
Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
6 # 1 Tim 1:16; Isa 55:6; Yn 7:34 Kwa hiyo kila mtu mtauwa
Akuombe wakati unapopatikana.
Hakika maji makuu yafurikapo,
Hayatamfikia yeye.
7 # Zab 9:9; Mit 18:10; Isa 4:6; Mt 23:37; Kol 3:3 Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso,
Utanizungusha nyimbo za wokovu.
8 # Isa 48:17 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;
Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
9Msiwe kama farasi wala nyumbu,
Walio hawana akili.
Kwa matandiko ya lijamu na hatamu
Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.
10 # Mit 13:21; Zab 34:8; Mit 16:20; Yer 17:7 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi,
Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka.
11Mfurahieni BWANA;
Shangilieni, enyi wenye haki
Pigeni vigelegele vya furaha;
Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 32: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia