Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 36

36
Uovu wa Watu na Wema wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi, mtumishi wa Bwana
1 # Rum 3:18; Mwa 20:11; Mit 8:13; Mhu 12:3 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake,
Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.
2Kwa maana hujipendekeza machoni pake
Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.
3 # Yer 4:22 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila,
Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.
4 # Mik 2:1; Isa 65:2 Huwaza maovu kitandani pake,
Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii.
5 # Zab 57:10 Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni,
Uaminifu wako hata mawinguni.
6 # Ayu 11:8; Rum 11:33; Ayu 7:20; Zab 145:9 Haki yako ni kama milima ya Mungu,
Hukumu zako ni vilindi vikuu,
Ee BWANA, unawaokoa wanadamu na wanyama.
7 # Rut 2:12 Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako!
Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
8 # Ayu 20:17; Ufu 22:1 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,
Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.
9 # Isa 12:3; Yer 2:13; Zek 13:1; Yn 4:10,14; Ufu 21:6; Mdo 26:18; Efe 5:8; Kol 1:13; 1 Pet 2:9 Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,
Katika nuru yako tutaona nuru.
10 # Yer 22:16 Uwadumishie wakujuao fadhili zako,
Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.
11Mguu wa kiburi usinikaribie,
Wala mkono wa wasio haki usinifukuze.
12Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu;
Wameangushwa chini wasiweze kusimama.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 36: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia