Zab 87
87
Shangwe ya Kuishi Sayuni
Ya Wakorahi. Zaburi. Wimbo.
1Msingi wake upo
Juu ya milima mitakatifu.
2BWANA ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko maskani zote za Yakobo.
3 #
Isa 60:1
Umetajwa kwa mambo matukufu,
Ee Mji wa Mungu.
4Nitataja Rahabu na Babeli
Miongoni mwao wanaonijua.
Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi;
Huyu alizaliwa humo.
5 #
Eze 48:35; Mt 16:18 Naam, mintarafu Sayuni itasemwa,
Huyu na huyu alizaliwa humo.
Na Yeye Aliye juu
Ataufanya imara.
6 #
Zab 22:30; Isa 4:3; Yer 3:19; Eze 13:9 BWANA atahesabu, awaandikapo mataifa,
Huyu alizaliwa humo.
7Waimbao na wachezao na waseme,
Visima vyangu vyote vimo mwako.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 87: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.