Rum 10
10
1 #
Mdo 22:3
Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. 2Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. 3#Rum 9:31,32Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. 4#Mt 5:17; Yn 3:18; Ebr 8:13Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Wokovu ni kwa Wote
5 #
Law 18:5; Gal 3:12 Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo. 6#Kum 30:12-14Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini), 7au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) 8#Kum 30:14Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. 9#2 Kor 4:5Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. 10Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. 11#Isa 28:16Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. 12#Mdo 10:34; 15:9Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; 13#Yoe 2:32kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. 14Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? 15#Isa 52:7Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
16 #
Isa 43:1
Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu? 17#Yn 17:20Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. 18#Zab 19:4Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia,
Sauti yao imeenea duniani mwote,
Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
19 #
Kum 32:21
Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena,
Nitawatia wivu kwa watu ambao si taifa,
Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhibisha.
20 #
Isa 65:1
Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema,
Nalipatikana nao wasionitafuta,
Nalidhihirika kwao wasioniulizia.
21 #
Isa 65:2
Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi.
Iliyochaguliwa sasa
Rum 10: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.