Matendo 9
9
Kuongoka kwa Sauli
1 #
Mdo 22:3-21; 26:9-20 Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, #Mdo 8:3 2akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, wanaume kwa wanawake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 3#1 Kor 15:8 Wakati alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafla nuru kutoka mbinguni ikamwangaza kotekote. 4Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona wanitesa? 5#Mdo 5:39 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayemtesa. 6Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. 7Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, waliisikia sauti, lakini hawakuona mtu. 8Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.
10 #
Mdo 10:17; 16:9 Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. 11#Mdo 21:39 Bwana akamwambia, Simama, nenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba; 12naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena. 13Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu; 14#1 Kor 1:2; Mdo 22:16; 2 Tim 2:22 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. 15#Rum 1:5; Mdo 25:13; 27:24; 2 Kor 4:7 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. 16#Mdo 23:29; 2 Kor 11:23-28 Maana nitamwonesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.
17Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. 18Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; 19akala chakula, na kupata nguvu.
Sauli ahubiri katika Dameski
Akawa huko siku kadhaa pamoja na wanafunzi walioko Dameski. 20Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. 21#Mdo 8:1; 9:1,14; 26:10 Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaua walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani? 22#Mdo 18:28 Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.
Sauli aokoka kuuawa na Wayahudi
23 #
2 Kor 11:32-33
Hata siku nyingi zilipopita, Wayahudi wakafanya shauri ili wamwue; #Mdo 23:12-29 24#Mdo 23:16 lakini hila yao ikajulikana na Sauli. Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua. 25Wanafunzi wake wakamtwaa usiku wakamshusha ukutani, wakimteremsha katika kapu.
Sauli akiwa Yerusalemu
26 #
Gal 1:17-19
Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. 27#Mdo 9:20 Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu. 28Naye akawa pamoja nao katika Yerusalemu akiingia na kutoka. 29Akahubiri kwa jina la Bwana kwa ushujaa, akinena na kuhojiana na Wayahudi wa Kigiriki. Nao wakajaribu kumwua. 30#Mdo 11:25; Gal 1:21 Lakini ndugu walipopata habari wakamchukua mpaka Kaisaria, wakamtuma aende Tarso.
31Basi kanisa likapata raha kote katika Yudea na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Kuponywa kwa Ainea
32Wakati Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote akawateremkia na watakatifu waliokaa Lida. 33Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo alikuwa amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. 34Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; inuka, ujitandikie. Mara akainuka. 35Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana.
Petro akiwa Lida na Yafa
36Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi#9:36 Jina Tabitha ni la Kiarameo, tafsiri yake katika Kigiriki ni Dorkasi. (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37Ikawa siku zile akaugua, akafa; wakati walipokwisha kumwosha, wakamweka ghorofani. 38Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi waliosikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Njoo kwetu pasipo kukawia. 39Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu ghorofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 40#Mk 5:40,41 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, inuka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. 41#Mdo 9:32 Akampa mkono, akamwinua; hata kisha akawaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, akiwa hai. 42Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana. 43#Mdo 10:6 Basi Petro akakaa siku kadhaa huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 9: SRUVDC
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.