Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 25

25
Waimbaji wa hekaluni
1 # 1 Nya 12:28; 23:2; 6:33; 15:17; Kut 15:20; Hes 11:25; 1 Sam 10:5; 1 Nya 16:4; 23:5; Zab 150:3,5; 1 Kor 14:1; Ufu 15:2,4 Tena Daudi na makamanda wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi kulingana na utumishi wao; 2wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme. 3Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu BWANA. 4Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi; 5#1 Sam 9:9; 2 Sam 24:11; 1 Nya 21:9; 26:28; Amo 7:12; 1 Pet 4:11; Mwa 33:5; 1 Sam 1:17; 1 Nya 28:5; Zab 127:3; 128:3; Isa 3:18 hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu. 6Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme. 7#Zab 150:1; Efe 5:19; Kol 3:16; Yak 5:13 Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia BWANA, wote waliokuwa mastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane. 8#2 Nya 23:13 Wakapigiwa kura ya huduma zao, kwa pamoja, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi. 9Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili; 10ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 11ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 12ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 13ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 14ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 15ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 16ya tisa Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili; 17ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 18ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 19ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 20ya kumi na tatu Shebueli, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 21ya kumi na nne Matithia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 22ya kumi na tano Yeremothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 23ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 24ya kumi na saba Yoshbekasha, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 25ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 26ya kumi na tisa Malothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 27ya ishirini Eliatha, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 28ya ishirini na moja Hothiri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 29ya ishirini na mbili Gidalti, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 30ya ishirini na tatu Mahaziothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 31#Ufu 4:4; 5:8; 11:16 ya ishirini na nne Romanti-ezeri, wanawe na nduguze, kumi na wawili.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mambo ya Nyakati 25: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia