Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 14:1-9

1 Wakorintho 14:1-9 SRUV

Ufuatilieni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kutoa unabii. Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake. Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo. Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali atoaye unabii hulijenga kanisa. Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kutoa unabii, maana yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa. Ila sasa, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya hotuba, au kwa njia ya fundisho? Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, ikiwa ni filimbi, ikiwa ni kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi? Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana, ni nani atakayejitayarisha kwa vita? Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu.