1 Samweli 2
2
Ombi la Hana
1 #
Lk 1:46-55; Flp 4:6; Zab 9:14; 13:5; 20:5 Naye Hana akaomba, akasema,
Moyo wangu wamshangilia BWANA,
Pembe yangu imetukuka katika BWANA,
Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu;
Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;
2 #
Kut 15:11; Isa 6:3; 57:15; Kum 4:35; Zab 73:25 Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA;
Kwa maana hakuna yeyote ila wewe,
Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
3 #
Mal 3:13
Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo;
Majivuno yasitoke vinywani mwenu;
Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa,
Naye huyapima matendo kwa mizani.
4Pinde zao mashujaa zimevunjika,
Na hao waliojikwaa wamepata nguvu.
5 #
Lk 1:53; Zab 113:9; Isa 54:1; Gal 4:27 Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula,
Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena.
Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba,
lakini aliye na watoto wengi amehuzunika.
6 #
Kum 32:39; Ayu 5:18; Hos 6:1; Yn 5:25-29; 11:25,26; Ufu 1:18 BWANA huua, naye hufanya kuwa hai;
Hushusha hadi kuzimu, tena huleta juu.
7 #
Ayu 1:21; 5:11; Zab 102:10; 75:7 BWANA hufukarisha mtu, na hutajirisha;
Hushusha chini, tena huinua juu.
8 #
Dan 4:17; Mwa 41:14; 1 Sam 15:17; Ayu 36:7; Yak 2:5; Ufu 1:6; 3:21; Ebr 1:3 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha mhitaji kutoka jaani,
Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu;
Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA,
Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
9 #
Zab 91:11; 1 Sam 14:6 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake;
Bali waovu watanyamazishwa gizani,
Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;
10 #
Zab 96:13
Washindanao na BWANA watapondwa kabisa;
Toka mbinguni yeye atawapigia radi;
BWANA ataihukumu dunia yote;
Naye atampa mfalme wake nguvu,
Na kuitukuza pembe ya masihi#2:10 Neno hili masihi, kwa Kiebrania, maana yake ni Mtiwa mafuta, au, Mwenye kuwekwa wakfu kwa kutiwa mafuta ili awe mfalme, au kuhani, au nabii. Kwa Kigiriki ni Kristo. wake.
Utovu wa wana wa Eli
11 #
1 Sam 3:1
Kisha Elkana akaenda Rama nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia BWANA mbele yake Eli, kuhani.
12 #
Kum 13:13; Rum 1:28 Basi, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali BWANA, 13wala haki ya makuhani ilivyokuwa kwa watu. Wakati huo mtu yeyote alipotoa dhabihu wakati wowote, ndipo huja mtumishi wa kuhani, nyama ilipokuwa katika kutokota, naye akawa na uma wa meno matatu mkononi mwake; 14naye huutia kwa nguvu humo chunguni, au birikani, au sufuriani, au chomboni; nyama yote iliyoinuliwa kwa huo uma kuhani huichukua mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokuja huko. 15Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, huja mtumishi wa kuhani, akamwambia yule mwenye kuitoa dhabihu, Mtolee kuhani nyama ya kuoka; kwa kuwa hataki kupewa nyama iliyotokoswa, bali nyama mbichi. 16Tena, ikiwa mtu yule amwambia, Hawakosi wataichoma moto hayo mafuta kwanza, kisha utwae kadiri roho yako itakavyopenda; ndipo husema, Sivyo, lakini sharti unipe sasa hivi; la, hunipi, basi nitaitwaa kwa nguvu. 17#Mwa 6:11; Mal 2:8; Rum 2:24 Hivyo dhambi yao wale vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa BWANA; kwa maana hao watu walidharau sadaka ya BWANA.
Mtoto Samweli akiwa Shilo
18 #
Kut 28:4
Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za BWANA, naye alikuwa kijana aliyevaa naivera ya kitani. 19Tena mamaye alimshonea kanzu ndogo, na kumletea kila mwaka, hapo alipokwea pamoja na mumewe ili kutoa dhabihu kila mwaka. 20Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, BWANA na akupe uzao kwa mwanamke huyu, wachukue mahali pa yule aliyemtoa kwa BWANA. Kisha wakarudi nyumbani kwao. 21#Mwa 21:1; Lk 2:40 Naye BWANA akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, watatu wa kiume na wawili wa kike. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za BWANA.
Unabii juu ya nyumba ya Eli
22Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania. 23Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote. 24Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa BWANA. 25#Hes 15:30; Kum 2:30; Mit 15:10; Yn 12:39,40 Mtu mmoja akimkosea mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosea BWANA, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu BWANA amekusudia kuwaua. 26#Lk 2:52; Mit 3:4; Lk 2:40; Mdo 2:47; Rum 14:18 Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia.
27 #
1 Fal 13:1; Kut 4:14 Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli, akamwambia, BWANA asema hivi, Je! Mimi sikujidhihirisha nafsi yangu kwa nyumba ya baba yako, walipokuwa katika Misri, wakiitumikia nyumba ya Farao? 28#Kut 28:1-4; Law 7:35-36; 2:3 Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa koo za baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto? 29#Kum 32:15; Mal 1:12; Kum 12:5 Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema? 30#1 Nya 15:2; Yer 18:9; Zab 18:20; 91:14; Yn 5:44; 12:26; 1 Pet 1:7; Hes 11:20; 2 Sam 12:9,10; Mal 2:9 Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nilisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau nitawadharau. 31#1 Sam 4:11 Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa watu wa ukoo wa baba yako, hata nyumbani mwako hapatakuwako mzee. 32#Zek 8:4 Nawe utayatazama mateso ya maskani yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hapatakuwako mzee milele. 33Tena mtu wako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa watakapokuwa watu wazima.#2:33 Tafsiri zingine zina ‘watauawa kwa upanga’. 34#1 Sam 4:11 Na yatakayowapata wana wako wawili, Hofni na Finehasi; ndiyo ishara itakayokuwa kwako; wote wawili watakufa siku moja. 35#1 Fal 2:35; 1 Nya 29:22; Ebr 2:17; 7:26-28; 2 Sam 7:11; 1 Fal 11:38; Zab 2:2 Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya kulingana na yale yaliyo katika moyo wangu na katika akili yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi#2:35 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wangu milele. 36#1 Fal 2:27 Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, apate kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali nitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate.
Iliyochaguliwa sasa
1 Samweli 2: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.