Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Timotheo 4

4
Kujinyima kusikofaa
1 # 2 Tim 3:1; 2 Pet 3:3; Yud 1:18; 1 Yoh 2:18 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3#Mwa 9:3; 1 Kor 10:30,31 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. 4#Mwa 1:31; Mdo 10:15 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Mtumishi mwema wa Yesu Kristo
6Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoefu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata. 7#1 Tim 1:4; 6:20; 2 Tim 2:16,23; Tit 1:14; 3:9 Bali hadithi za kale, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. 8#1 Tim 6:6 Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
9 # 1 Tim 1:15 Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa; 10#1 Tim 2:3,4 kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa wale waaminio.
11Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha. 12#Tit 2:15 Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. 13Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma Maandiko, kuonya na kufundisha. 14#1 Tim 5:22; 2 Tim 1:6; Mdo 6:6; 8:17 Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono na wazee. 15Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. 16#Rum 11:14 Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako, na wale wakusikiao pia.

Iliyochaguliwa sasa

1 Timotheo 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia