Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mambo ya Nyakati 25

25
Utawala wa Amazia
1 # 2 Fal 14:1 Amazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na tisa; na jina la mamaye aliitwa Yehoadani wa Yerusalemu. 2#2 Fal 14:4; Isa 29:13; Hos 10:2 Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, lakini si kwa moyo mkamilifu. 3#2 Fal 14:5 Basi ikawa, alipojiimarisha katika ufalme wake, akawaua watumishi wale waliomwua mfalme babaye. 4#Kum 24:16; 2 Fal 14:6; Yer 31:30; Eze 18:20 Lakini watoto wao hakuwaua, ila alifanya kulingana na hayo yaliyoandikwa katika Torati, katika kitabu cha Musa, kama BWANA alivyoamuru, akisema, Wazazi wasiuawe kwa ajili ya dhambi ya watoto wao wala watoto wasiuawe kwa ajili ya dhambi ya wazazi; lakini kila mtu atakufa kwa dhambi yake mwenyewe.
Kuuawa kwa Waedomi
5 # Hes 1:3 Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka kulingana na nyumba za baba zao chini ya makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule elfu mia tatu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao. 6Akaajiri pia watu mashujaa elfu mia moja wa Israeli kwa talanta#25:6 Talanta moja ni kama kilo 34. mia moja za fedha. 7#2 Nya 15:2; 1 Fal 12:28; Isa 28:1-3; Hos 4:6-19; 5:6-15; 9:11-17 Lakini mtu wa Mungu akamjia, akasema, Ee mfalme, usiwaruhusu jeshi la Israeli waende nawe; kwa kuwa BWANA hayupo pamoja na Israeli, yaani, wana wote wa Efraimu. 8#Mwa 18:14; Amu 7:7; 1 Sam 14:6; 1 Nya 29:11; 2 Nya 14:11; 20:6; Ayu 5:18; 42:2; Zab 20:7; 118:6; Yer 32:17; Mt 19:26; Rum 8:31 Lakini ukitaka kwenda, haya, jitie nguvu upigane; Mungu atakuangusha mbele ya adui; maana Mungu anazo nguvu za kusaidia, na kuangusha. 9#Kum 8:18; 2 Nya 1:12; Mit 10:22; Hag 2:8 Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta#25:9 Tazama 2 Nya. 25:6. mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, BWANA aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo. 10Ndipo Amazia akaachilia jeshi lililomjia kutoka Efraimu, ili warudi kwao; kwa hiyo hasira yao ikawaka sana juu ya Yuda, nao wakarudi kwao wenye hasira kali. 11#2 Fal 14:7 Amazia akapiga moyo konde, akawaongoza watu wake, akaenda mpaka Bonde la Chumvi, akawapiga katika wana wa Seiri watu elfu kumi. 12Na elfu kumi wengine, ambao wana wa Yuda waliwachukua wakiwa hai, wakawaleta juu ya jabali, wakawaangusha chini toka juu ya jabali, hadi wakavunjikavunjika wote. 13Lakini wanajeshi, aliowarudisha Amazia, wasiende naye vitani, hao wakaiteka miji ya Yuda, tangu Samaria mpaka Beth-horoni, wakawapiga watu elfu tatu, wakachukua nyara nyingi.
14 # 2 Nya 28:23; Kut 20:3,5 Basi ikawa, Amazia alipokwisha rudi kutoka kuwaua Waedomi, alileta miungu ya wana wa Seiri, akaisimamisha kuwa miungu yake, akaisujudia, akaifukizia uvumba. 15#Zab 96:5; 115:3-8; Isa 46:1,2; Yer 10:3-5; Mdo 19:26; 1 Kor 8:4 Kwa hiyo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Amazia, akamtuma kwake nabii, aliyemwambia, Mbona umeitafuta miungu ya watu, isiyowaokoa watu wao mkononi mwako? 16#2 Nya 16:10; Mit 9:7,8; 2 Tim 4:3; 1 Sam 2:25 Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.
Israeli wawashinda Yuda
17 # 2 Fal 14:8,9 Ndipo mfalme Amazia akafanya shauri, akatuma wajumbe kwa Yehoashi,#25:17 Au, Yoashi. mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli, kusema, Njoo, tutazamane uso kwa uso. 18Na Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amazia mfalme wa Yuda, kusema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ukatuma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita mnyama wa mwituni aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti. 19#2 Nya 35:21; Mit 12:15; 18:6 Wasema, Tazama, umewapiga Edomu; na moyo wako wakutukuza ujisifu; kaa nyumbani mwako basi; mbona unataka kujitia bure katika madhara, hata uanguke, wewe na Yuda pamoja nawe? 20#1 Fal 12:15; 2 Nya 22:7 Lakini Amazia hakutaka kusikia, kwa maana hayo yalitoka kwa Mungu, ili awatie mikononi mwao, kwa kuwa wameitafuta miungu ya Edomu. 21Basi Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea; wakatazamana uso kwa uso, yeye na Amazia mfalme wa Yuda huko Beth-shemeshi, ulio wa Yuda. 22Yuda wakashindwa na Israeli; wakakimbia kila mtu hemani kwake. 23#2 Nya 21:17; 22:1,6 Yehoashi mfalme wa Israeli akamtwaa Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia,#25:23 Yehoahazi. huko Beth-shemeshi, akamchukua mpaka Yerusalemu, akauvunja ukuta wa Yerusalemu, toka lango la Efraimu mpaka Lango la Pembeni, dhiraa mia nne. 24Akaitwaa dhahabu yote, na fedha, na vyombo vyote vilivyoonekana nyumbani mwa Mungu kwa Obed-edomu, na hazina za nyumba ya mfalme, tena watu kuwa amana, akarudi Samaria.
Kifo cha Amazia
25 # 2 Fal 14:17 Naye Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, akaishi miaka kumi na mitano baada ya kufa kwake Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli. 26Na mambo yote ya Amazia yaliyosalia, ya kwanza hadi mwisho, tazama, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli? 27Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata BWANA, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko. 28#2 Fal 14:20 Wakamleta juu ya farasi; wakamzika pamoja na babaze katika mji wa Yuda.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mambo ya Nyakati 25: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia