Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mambo ya Nyakati 9

9
Ziara ya malkia wa Sheba
1 # 1 Fal 10:1; Mt 12:42; 13:11,35; Lk 11:31; Zab 49:4; 78:2; Mit 1:5; Eze 20:49 Na malkia wa Sheba aliposikia sifa za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, akiwa na wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake. 2Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno alilofichiwa Sulemani, asimwambie. 3Naye malkia wa Sheba alipoona hekima ya Sulemani, na nyumba aliyoijenga, 4na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha maofisa wake, na huduma ya watumishi wake na mavazi yao; pia wanyweshaji wake na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya BWANA; roho yake ilizimia. 5Akamwambia mfalme, Habari zile nilizozisikia katika nchi yangu zihusuzo mambo yako na hekima yako ni za kweli. 6Lakini mimi sikuyasadiki maneno yao, hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu; wala, tazama, ukuu wa hekima yako sikuambiwa nusu; wewe umezidi kuliko habari nilizozisikia. 7Heri watu wako, na heri hawa watumishi wako, wasimamao mbele yako sikuzote, wakisikia hekima yako. 8#Zab 72:18,19 Na ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti chake cha enzi, kuwa mfalme wake BWANA, Mungu wako; kwa kuwa Mungu wako amewapenda Israeli, kuwathibitisha milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme juu yao, ufanye hukumu na haki. 9Basi akampa mfalme talanta mia moja na ishirini za dhahabu, na manukato mengi mengi sana, na vito vya thamani; wala hapakuwapo manukato mengi kama hayo aliyopewa mfalme Sulemani na malkia wa Sheba. 10#1 Fal 5:2-6; 9:27,28; 2 Nya 8:18; Zab 72:10; 1 Fal 10:11 Tena watumishi wa Hiramu, pamoja na watumishi wa Sulemani, walioleta dhahabu kutoka Ofiri, wakaleta miti ya msandali, na vito vya thamani. 11Mfalme akatengeneza kwa miti hiyo ya msandali madari ya nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haijatokea kama hiyo katika nchi ya Yuda. 12Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichokitaka na zaidi ya vile alivyomletea mfalme. Basi akarudi, akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Ukwasi wa Sulemani
13Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani mwaka mmoja, ni talanta mia sita sitini na sita za dhahabu; 14#Zab 68:29; 72:10; Isa 45:14; 60:6; Yer 25:24 mbali na ile waliyoileta wachuuzi na wafanya biashara; tena wafalme wote wa Arabuni, na watawala wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha. 15Mfalme Sulemani akafanya ngao mia mbili za dhahabu iliyofuliwa; ngao moja hupata shekeli mia sita za dhahabu iliyofuliwa. 16Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kigao kimoja hupata shekeli mia tatu za dhahabu; mfalme akaviweka katika nyumba ya msitu wa Lebanoni. 17Tena mfalme akafanya kiti cha enzi kikubwa cha pembe, akakifunikiza kwa dhahabu iliyo safi. 18Kiti kile kilikuwa na ngazi sita, tena na kikao cha miguu cha dhahabu, navyo vilikuwa vimeshikamana na kiti; na kila upande wa kiti hicho palikuwa na pakuengemeza mikono, na simba wawili walisimama kando ya hiyo mikono. 19Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya ngazi sita pande zote; wala mfano wake ulikuwa haujawahi kutengenezwa katika ufalme wowote ule. 20Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi; fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani. 21#1 Fal 10:22; 22:48; Zab 48:7; 72:10; Isa 2:16; 60:9; Yer 10:9; Yon 1:3 Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu zilizokwenda Tarshishi pamoja na watumishi wa Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi. 22#1 Fal 3:12,13; 10:23,24; Zab 89:27; Mt 12:42; Kol 2:2,3 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima. 23Wafalme wote wa duniani wakamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni. 24#Zab 72:10,15 Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, kwa wingi kila mwaka. 25#1 Fal 4:26; 10:26; 2 Nya 1:14 Sulemani akawa na mazizi ya farasi na magari elfu nne, na wapandao farasi elfu kumi na mbili, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. 26#1 Fal 4:21; Mwa 15:18; Zab 72:8 Akatawala juu ya wafalme wote toka Mto#9:26 Mto ni ‘Frati’. hadi nchi ya Wafilisti, na hadi mpaka wa Misri. 27#1 Fal 10:27; 2 Nya 1:15 Mfalme akafanya fedha humo Yerusalemu kuwa kama mawe, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi. 28#Kum 17:16; 1 Fal 4:26; 10:26,28; 2 Nya 1:16; Isa 2:7; 31:1 Wakamletea Sulemani farasi kutoka Misri, na kutoka nchi zote.
Kifo cha Sulemani
29 # 1 Fal 11:29,41; 2 Nya 12:15; 13:22 Basi mambo yake Sulemani yaliyosalia, tangu mwanzo hadi mwisho je! Hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu la Nathani nabii, katika unabii wa Ahiya, Mshiloni, na katika maono ya Ido mwonaji ambayo yahusu Yeroboamu mwana wa Nebati? 30#1 Fal 11:42,43 Sulemani akatawala katika Yerusalemu juu ya Israeli wote miaka arubaini. 31Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa mjini mwa Daudi babaye; Rehoboamu mwanawe akatawala badala yake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mambo ya Nyakati 9: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia