Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wakorintho 6

6
1 # 2 Kor 1:24; 5:20 Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. 2#Isa 49:8; Lk 4:19,21 (Kwa maana asema,
Kwa wakati uliokubalika nilikusikia,
Na katika siku ya wokovu nilikusaidia;
tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.) 3Tusiwe kwazo la namna yoyote katika jambo lolote, ili utumishi wetu usilaumiwe; 4#2 Kor 4:2 bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika subira nyingi, katika mateso, katika shida, katika matatizo; 5#Mdo 16:23; 2 Kor 11:23-27 katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; 6#1 Tim 4:12 katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki; 7#1 Kor 2:4 katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kulia na za mkono wa kushoto; 8kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; 9#2 Kor 4:10; Zab 118:18 kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; 10#Flp 4:12,13 kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
11 # Zab 119:32 Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa. 12Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu. 13#1 Kor 4:14 Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo.
Hekalu la Mungu aliye hai
14 # Efe 5:11 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?#6:15 Beliari: maana yake ni, Ufisadi. Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16#Law 26:12; Eze 37:27; 1 Kor 3:16; 6:19; Eze 37:27 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17#Isa 52:11; Yer 51:45; Eze 20:34,41; Ufu 18:4 Kwa hiyo,
Tokeni kati yao,
Mkatengwe nao, asema Bwana,
Msiguse kitu kilicho kichafu,
Nami nitawakaribisha.
18 # 2 Sam 7:8,14; 1 Nya 17:13; Isa 43:6; Yer 31:9; 32:38; Hos 1:10; Amo 4:13 Nitakuwa Baba kwenu,
Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,
asema Bwana Mwenyezi.

Iliyochaguliwa sasa

2 Wakorintho 6: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia