Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Yohana UTANGULIZI

UTANGULIZI
Yohana alipata habari kuwa waalimu wa uongo waliendeleza mafundisho yao katika kanisa; hivyo akaandika Waraka huu kuagiza Wakristo wajitenge na walimu wa uongo na wasiwakaribishe katika ibada zao.
Mwandishi anajiita “Mzee” anayemwandikia “Bimkubwa” mteule pamoja na “Wanawe”. Mwandishi wa Waraka huu ni Yohana ambaye wakati huo, kiumri, alikuwa mzee aliyeheshimiwa kama Kiongozi wa kanisa (tazama utangulizi wa Waraka wa Kwanza wa Yohana). Walengwa wa Waraka huu ni kanisa fulani katika Asia Ndogo lililokuwa chini ya uongozi wake. Limepewa jina la heshima la “Bimkubwa mteule.” “Watoto wake” ni waumini waliokuwa katika kanisa hilo.
Mwandishi anawatahadharisha waumini waepuke mafundisho ya uongo, wazingatie imani, ukweli na upendo.

Iliyochaguliwa sasa

2 Yohana UTANGULIZI: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia