Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 8

8
Ushindi wa Daudi
1 # 2 Sam 7:9; 21:15-22; 1 Nya 18:1 Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti. 2#Hes 24:17; 1 Sam 14:47; Zab 60:8; 72:10 Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi. 3#2 Sam 10:6; Mwa 15:18 Tena Daudi akampiga Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kujipatia tena mamlaka yake huko Mtoni. 4Daudi akampokonya wapanda farasi elfu moja na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia moja akawabakiza. 5Na Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akawapiga watu elfu ishirini na mbili wa Washami. 6Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda. 7Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumishi wa Hadadezeri, akazileta Yerusalemu. 8Tena toka Tebhathi na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno. 9Na Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia ya kwamba Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri, 10Tou akamtuma Yoramu mwanawe kwa mfalme Daudi ili kumsalimia, na kumpongeza, na kumbariki, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake Yorabu akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba; 11#1 Fal 7:51; 1 Nya 18:11; 22:14-16; Mik 4:13; Ufu 21:24 hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa BWANA, pamoja na hiyo fedha, na dhahabu alizofanya wakfu za mataifa yote aliowashinda; 12za Edomu, na za Moabu, na za wana wa Amoni, na za Wafilisti, na za Amaleki, na za nyara za Hadadezeri, mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba. 13#Zab 60:1; 2 Fal 14:7 Basi Daudi akajipatia jina, alipokuwa akirudi, aliwaua Waedomi elfu kumi na nne katika bonde la chumvi. 14#Mwa 27:29; Hes 24:18; Zab 37:28; 121:8; 145:20 Akaweka askari wenye kulinda ngome katika Edomu; katikati ya Edomu yote akaweka ngome, na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye BWANA akampa Daudi ushindi kila kokote alikokwenda.
Wakuu wa Daudi
15Daudi akatawala juu ya Israeli wote; naye Daudi akawafanyia hukumu na haki watu wake wote. 16#2 Sam 19:13; 1 Fal 4:3 Huyo Yoabu, mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa majeshi; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, mwekaji kumbukumbu;#8:16 Katika Kiebrania ni mwenye kuandika tarehe. 17#1 Nya 24:3 na Sadoki, mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi; 18#1 Nya 18:17; 1 Sam 30:14 na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi wakawa makuhani.

Iliyochaguliwa sasa

2 Samweli 8: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia