2 Samweli UTANGULIZI
UTANGULIZI
Kitabu hiki kinaendeleza masimulizi ya Kitabu cha Kwanza cha Samweli kuhusu mfalme Daudi (angalia utangulizi wa Kitabu cha Kwanza cha Samweli). Daudi ni mtawala maarufu. Wakati wa utawala wake, Israeli limekuwa taifa moja na lenye nguvu. Daudi anaonekana kuwa mwenye imani thabiti na kumcha Mungu. Hata hivyo, udhaifu wake haukufichwa pia (11:1—12:12).
Masimulizi ya kitabu hiki yana mkazo kuwa uwezo na mamlaka vyenye kufaulu hutoka kwa Mungu. Kiongozi wa Israeli aliongoza kwa niaba ya Mungu na aliwajibika kwa Mungu. Hivyo badiliko la kutoka uongozi wa waamuzi kuwa uongozi wa kifalme lilipata kibali cha Mungu (1 Sam 8:7,22).
Yaliyomo:
1. Utangulizi wa utawala wa Daudi, Sura 1—4
2. Ufalme wa Israeli ukiongozwa na Mfalme Daudi; Sura 5—10
3. Mfalme Daudi na Bathsheba, Sura 11—12
4. Balaa katika familia ya Daudi, Sura 13—20
5. Simulizi la nyongeza, Sura 21—24
Iliyochaguliwa sasa
2 Samweli UTANGULIZI: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.