Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 22

22
1 # Mdo 7:2; 13:26 Akasema, Enyi wanaume, ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea mbele yenu sasa.
2 # Mdo 21:40 Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema, 3#Mdo 9:1-29; 26:9-20 Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nilizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihada kubwa kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; #Mdo 5:34-39; Rum 10:2 4#Mdo 8:3; 26:9-11 nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake. 5Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nilipokea barua kutoka kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski, ili niwalete wale waliokuwa huko hadi Yerusalemu, wakiwa wamefungwa, ili waadhibiwe.
Paulo asema juu ya kuongoka kwake
6Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafla nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote. 7Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi? 8Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. 9Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami. 10Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye. 11Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fahari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikaingia Dameski. 12Basi mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi wote waliokaa huko, 13Akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu yangu Sauli, pata kuona tena. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile. 14#Mdo 3:14 Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake. 15Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. 16#2 Tim 2:22 Basi sasa, mbona unakawia? Simama, ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako, ukiliitia jina lake.
Paulo atumwa kwa Wamataifa
17 # Mdo 9:26; 11:30; Gal 1:18,19 Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemu, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa katika hali ya kuzimia roho, 18nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako kuhusu habari zangu. 19#Mdo 22:4 Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nilikuwa nikiwafunga gerezani wale wanaokuamini na kuwapiga katika kila sinagogi. 20#Mdo 7:58; 8:1 Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua. 21#Mdo 9:15; 13:2 Naye akaniambia, Nenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa Mataifa.
Paulo na Jemadari wa Kirumi
22 # Mdo 21:35 Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika nchi, kwa maana haifai aishi.
23Walipokuwa wakipiga kelele na kutupa mavazi yao na kurusharusha mavumbi juu, 24yule jemadari akaamuru aletwe ndani ya ngome, akisema aulizwe habari zake kwa kupigwa mijeledi, ili ajue sababu hata wakampigia kelele namna hii. 25#Mdo 16:37; 23:27 Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule ofisa aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado? 26Yule jemadari aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi. 27Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo. 28Jemadari akajibu, Mimi nilipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa. 29Basi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari naye akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.
Paulo mbele ya baraza
30Kesho yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru wakuu wa makuhani na baraza yote wakutane. Akamleta Paulo chini, akamweka mbele yao.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo 22: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia