Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Torati 1

1
Kumbukumbu ya yaliyotokea Horebu
1 # Hes 32:6,20,29; Yos 9:1; 22:4,7 Haya ndiyo maneno Musa aliyowaambia Israeli wote ng'ambo ya Yordani nyikani, katika Araba lililoelekea Sufu, kati ya Parani, na Tofeli, na Labani, na Hazerothi, na Dizahabu. 2#Hes 13:26; Kum 9:23 Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea. 3#Hes 33:38 Ikawa mwaka wa arubaini, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa akawaambia wana wa Israeli kama yote aliyopewa na BWANA ya kuwaamuru; 4#Hes 21:21-35; Neh 9:22; Zab 135:11; 139:19 alipokwisha kumpiga Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa akikaa Ashtarothi iliyo katika Edrei; 5ni ng'ambo ya Yordani katika nchi ya Moabu, alipoanza Musa kufunua torati hii, akisema, 6#Kut 3:11; 9:1; Hes 10:11 BWANA, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mmekaa katika mlima huu vya kutosha; 7geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati. 8#Mwa 12:7; 15:18; 28:13 Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.
Viongozi wa makabila wateuliwa
9 # Kut 18:18; Hes 11:14 Nami wakati ule niliwaambia, nikasema, Mimi siwezi kuwachukua peke yangu. 10#Mwa 15:5; 22:17; 28:14; Kut 32:13; Kum 10:22; 28:62; 1 Nya 27:23 BWANA, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi. 11#Mwa 22:17; 26:4; Kut 32:13 BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabariki, kama alivyowaahidi. 12#1 Fal 3:8; 2 Kor 11:28 Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na ugomvi wenu? 13Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya makabila yenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu. 14Nanyi mkanijibu, mkaniambia, Jambo ulilolisema ni jema la kufanya. 15Basi nikatwaa vichwa vya makabila yenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, na makamanda wa hamsini hamsini, na makamanda wa kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya makabila yenu. 16#Kut 23:2-8; Yn 7:24; Law 24:22 Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikilizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye. 17#1 Sam 16:7; Mit 24:23; Yak 2:1; Mit 28:21; 29:4,25; 2 Nya 19:6; Kut 18:22,26 Msitazame nafsi za watu katika hukumu; muwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu yeyote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza. 18Nikawaamuru wakati huo mambo yote yaliyowapasa ninyi kuyafanya.
Waisraeli wakataa kuingia katika nchi
19 # Hes 10:12; Kum 8:15; Yer 2:6; Hes 13:26 Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama BWANA, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea. 20Nami nikawaambia, Mmefika nchi ya vilima ya Waamori, anayotupa sisi BWANA, Mungu wetu. 21#Hes 13:30; 14:8,9; Yos 1:9; Zab 27:1-3; 46:1,7,11; Isa 41:10; 43:1,2; Lk 12:32; Ebr 13:6 Tazama, BWANA, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike. 22Nanyi mkanikaribia kila mmoja wenu, mkasema, Na tutume watu mbele yetu, ili watupelelezee nchi na kutuletea habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia. 23#Hes 13:3 Neno hili likanipendeza sana; nikatwaa watu kumi na wawili, mtu mmoja wa kila kabila. 24Nao wakageuka, wakapanda mlimani wakafika katika bonde la Eshkoli, wakalipeleleza. 25Wakachuma baadhi ya matunda ya nchi ile mikononi mwao, wakatuletea huku chini, wakatuletea habari tena, wakasema, Nchi hii anayotupa BWANA, Mungu wetu, ni nchi njema.
26 # Kum 9:23; Ebr 3:16; Hes 14:1-4; Zab 106:24 Lakini hamkukubali kukwea huko, mliasi neno la BWANA, Mungu wenu; 27#Kum 9:28 mkanung'unika hemani mwenu, mkasema, Ni kwa sababu BWANA ametuchukia, ndipo akatutoa katika nchi ya Misri, apate kututia katika mikono ya Waamori, ili kutuangamiza. 28#Hes 13:28-33; Kum 9:1,2 Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni wengi, ni warefu kuliko sisi; miji nayo ni mikubwa, imejengewa kuta hata mbinguni; na zaidi ya hayo huko tumewaona Waanaki. 29Ndipo nikawaambia msiwaogope. 30#Kut 14:14; Neh 4:20 BWANA, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu; 31#Mdo 13:18; Kut 19:4; Kum 32:11; Isa 46:3,4; 63:9; Hos 11:3 na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua BWANA, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafika mahali hapa.
32 # Ebr 3:19; Zab 106:24; Yud 1:5 Lakini katika jambo hili hamkumwamini BWANA, Mungu wenu, 33#Kut 13:21; Zab 78:14; Hes 10:33; Eze 20:6 aliyewatangulia njiani, usiku kwa moto, kuwaonesha njia mtakayoiendea, na mchana kwa hilo wingu, ili apate kuwatafutia mahali pa kusimamisha hema zenu.
Adhabu kwa ajili ya uasi wa Israeli
34 # Ebr 3:18; Kum 2:14 BWANA akaisikia sauti ya maneno yenu, akaghadhibika, akaapa, akasema, 35#Hes 14:22; Zab 95:11 Hakika yangu hapana mmoja miongoni mwa watu hawa wa kizazi hiki kibaya atakayeiona nchi hiyo nzuri, niliyowaapia baba zenu kuwapa, 36isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, huyo ataiona; nami nitampa yeye na watoto wake nchi hiyo aliyoikanyaga; kwa kuwa amemfuata BWANA kwa kila neno. 37#Hes 27:14; Kum 3:26; 4:21; 34:4; Zab 106:32 Na BWANA alinikasirikia mimi kwa ajili yenu, akasema, Wala wewe hutaingia humo; 38#Kut 24:13; 33:11; 1 Sam 16:22; Kum 31:7,23 Yoshua mwana wa Nuni asimamaye mbele yako ndiye atakayeingia; mtie moyo; kwa kuwa yeye atawarithisha Israeli. 39#Isa 7:15,16; Eze 18:20 Tena, wadogo wenu, mliosema watakuwa mateka, na wana wenu, wasiokuwa leo na maarifa ya mabaya wala mema, ndio watakaoingia, nao ndio nitakaowapa, nao wataimiliki. 40Na ninyi basi geukeni, mshike safari yenu, mwende jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu. 41Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya BWANA, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na BWANA. Mkajihami kila mtu silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani. 42BWANA akaniambia, Waambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi siko kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu. 43#Hes 14:44,45 Hata ingawa niliwaambia, hamkunisikiza, bali mliasi amri ya Bwana, makajiamini na kulewa mlimani. 44#Kum 28:25; 32:30; Zab 118:12; Isa 7:18 Na Waamori waliokuwa wakikaa katika mlima huo, waliwatokea juu yenu, wakawafukuza, kama wafukuzwao na nyuki, wakawapigia Seiri mpaka Horma. 45#Ayu 27:9; Zab 66:18; Mit 1:24; Isa 1:15; Yer 11:7-14; Zek 7:11; Yn 9:31 Mkarudi mkalia mbele za BWANA; BWANA asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu.
Maisha ya jangwani
46 # Hes 13:25; 20:1,22; Amu 11:17 Ndipo mkakaa Kadeshi siku nyingi, kwa kadiri ya hizo siku mlizokaa.

Iliyochaguliwa sasa

Kumbukumbu la Torati 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia